Mashabiki wa klabu ya Liverpool siku ya Juzi waliutumia
mwanya walioupata kwenye mchezo wa ligi dhidi ya timu ya Stoke City kwa
kupeperusha bango kubwa lilionesha kutoridhika kwao kwa kitendo cha
kupandishiwa bei ya tiketi kwenye michezo ya klabu hiyo.
Mashabiki hao walilionesha bango hilo lililoonesha namna
ambavyo bei ya tiketi kwa klabu yao imekua ikipanda kwa ghafla tangu mwaka wa
1990 mpaka kufikia hivi sasa.
Kwenye bango hilo mashabiki hao walionesha kuwa bei ya
tiketi ya kuwashuhudia majogoo hao wa Anfield ilikua paundi 4 mnamo mwaka 1990,
ambayo ilipanda mpaka kufikia kiasi cha paundi 24 mnamo mwaka 2000 na sasa
ghalama hiyo imepanda mpaka kufikia kiasi cha paundi 43 mnamo mwaka 2010 mpaka
sasa.
No comments:
Post a Comment