Pages

Wednesday, December 3, 2014

UWEZO WA VYUO VIKUU KUCHUKUA WANAFUNZI WA SAYANSI BADO CHANGAMOTO KWA TANZANIA KUTIMIZA MALENGO YA EFA‏

DSC_0341
Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi nchini Tanzania Mh. Dkt. Shukuru Kawambwa akifungua mkutano wa kimataifa wa kutathmini mafanikio na changamoto za utekelezaji wa malengo ya Mpango wa Kimataifa wa Elimu kwa Wote-EFA uliofanyika jijini Dar Es Salaam ambapo amesema tangu mwaka 2000 Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuelekea kutimiza malengo ya Mpango huo ikiwa ni utashi wa kisiasa na kuwajibika vikisaidiwa na kujitolea kwa wadau wa sekta ya elimu pamoja na washirika wa maendeleo.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog)


Na Mwandishi wetu
Tanzania imekuwa moja wapo ya nchi za kutolea mfano miongoni mwa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara katika kutekeleza maazimio ya mpango wa Elimu kwa wote (EFA)
Akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa wadau wote wa elimu , Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi nchini Tanzania Mh. Dkt. Shukuru Kawambwa amesema Tanzania Bara na Visiwani imeweza kukaribia kufikia malengo ya mpango huo ikiwa ni pamoja na suala la wastani wa waalimu kwa wanafunzi.
Amesema kwamba kwa shule za msingi Tanzania Bara imefikia wastani wa wanafunzi 47 kwa mwalimu mmoja wakati Visiwani Zanzibar ni wastani wa mwalimu mmoja kwa wanafunzi 27.
Mafanikio mengine yaliyopatikana chini ya mpango huo ni kuboresha wastani wa wanafunzi kwa darasa, ambapo kwa Tanzania Bara wastani umetoka kuwa wanafunzi 92 kwa darasa na sasa ni wanafunzi 65 huku Zanzibar wastani ukiwa ni wanafunzi 62 kwa darasa.
DSC_0288
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza wakati wa mkutano wa kimataifa wa kutathmini mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika kutekeleza malengo ya Mpango wa Kimataifa wa Elimu kwa Wote –EFA ulioshirikisha wadau wote wa sekta ya elimu uliofanyika jijini Dar Es Salaam. Amesema lengo kuu la mkutano huo ni kuiandaa Tanzania kuweza kushiriki kikamilifu katika mashauriano ya kiserikali baina nchi mbalimbali na kuhakikisha wadau wakuu wa elimu kitaifa wanapata taarifa juu ya mapendekezo ya agenda zitakazoanza mwaka 2015.
Awali Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues amesema ikumbukwe kwamba malengo nane (8) ya EFA yanachangia kufanikisha Malengo Makuu ya Maendeleo ya Millennia (MGDs) yaliyopitishwa mwaka 2000 kati ya nchi 189 na Taasisi za Mendeleo zinazoongoza Duniani.
Bi. Rodrigues amefafanua kuwa tunapoelekea mwaka 2015, Tanzania Bara na Visiwani zimeonyesha juhudi katika kupunguza tofauti kubwa zilizokuwepo kielimu ikiwa ni pamoja na kukabilia na changamoto zilizojitokeza na kuweza kuweka sera, mipango na utawala bora katia Nyanja za fedha , wadau, usimamizi na uwajibikaji.
DSC_0224
Pichani juu na chini ni sehemu ya wadau wa elimu kutoka bara na visiwani wakifuatilia hotuba za viongozi wakati wa mkutano wa kimataifa wa kutathmini mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika kutekeleza malengo ya Mpango wa Kimataifa wa Elimu kwa Wote –EFA.
Katika mkutano huo imeelezwa kwa sasa hakuna tatizo la uwiano wa wanafunzi wa kike na wa kiume kwa kuwa jinsia zote zipo darasani katika uwiano unaoridhisha unaokaribia wastani wa 50/50, lakini pia kigezo kingine ni uwiano wa idadi ya wanafunzi wanaojiunga na sekondari ambapo bado kumeonyesha kuwa na mapungufu hivyo kazi ya ziada inahitajika.
Mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam ulikuwa na nia ya kutoa fursa kwa nchi wahusika kujitathimini zimefikia wapi katika utekelezaji wa malengo waliyojiweke ya Mpango wa Elimu kwa Wote-EFA kwa kipindi cha mwaka 2000 hadi 2015 na kujiwekea mikakati mipya.
DSC_0280 DSC_0470 DSC_0236 DSC_0364 DSC_0489
Kamishna wa Elimu kutoka Wizarani, Prof. Eustella Bhalalusesa (wa pili kushoto) akitoa maoni juu changamoto zinazolikabili taifa katika kuleta uwiano kwenye ya sekta elimu.
DSC_0476
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues akishea uzoefu wake katika utekelezaji wa malengo ya EFA baina ya Tanzania na nchi zingine za Afrika.
DSC_0371
DSC_0491
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Maalim Abdallah M. Abdallah (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues wakati wa mkutano huo. Kushoto ni Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi nchini Tanzania Mh. Dkt. Shukuru Kawambwa.
DSC_0501
Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi nchini Tanzania, Mh. Dkt. Shukuru Kawambwa akifurahi jambo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues baada ya kumalizika kwa mkutano huo.
DSC_0505
Mkurugenzi wa ofisi ya elimu kutoka Shirika la USAID, Bw. David Bruns (kushoto) akibadilishana mawazo na Waziri Kawambwa (katikati) na Bi. Zulmira Rodrigues.
DSC_0512
Afisa Miradi Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO, Myoung Su Ko akiteta jambo na Afisa mipango ya Elimu wa Shirika la UNESCO, Bi. Jennifer Kotta.
DSC_0457
Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi nchini Tanzania Mh. Dkt. Shukuru Kawambwa, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na nafasi ya Tanzania ilipofikia tangu 2000-2015 katika utelekezaji wa malengo ya EFA.
DSC_0429
Afisa mipango ya Elimu wa Shirika la UNESCO, Bi. Jennifer Kotta akizungumza na waandishi wa habari juu ya umuhimu wa mkutano huo baina ya UNESCO na Wizara katika kutathmini utelekezaji wa malengo ya EFA katika kipindi cha miaka 15 na kutoa nafasi ya kujipanga kwa awamu nyingine itakayoanza 2015-2030.

No comments:

Post a Comment