Jolly Tumuhirwe ameomba mahakama kumsamehe kwa kumtesa mtoto
Mfanyakazi wa nyumbani aliyenaswa kwenye kanda ya video
akimchapa na kumkanyaga mtoto nchini Uganda, amefikishwa mahakamani leo.
Mfanyakazi huyo Jolly Tumuhirwe aliambia mahakama kuwa
anajulia kile alichokifanya na hata kuomba msamaha. Ameshitakiwa kwa kosa la
kumtesa mtoto Arnella.
Licha ya taarifa ya polisi kusema Jolly atashitakiwa kwa
kosa la jaribio la ,mauaji, kiogozi wa mashitaka
alimshitaki Jolly kwa kosa la
kumtesa mtoto mdogo.
Bi Tumuhirwe alikiri makosa yake na kuomba msamaha. Hakuna
wakili yeyote aliyemwakilisha Jolly mahakamani licha ya mmoja wa mawakili
mashuhuri kusema angemwakilisha Jolly bila malipo.
Kesi hio imeakhirishwa hadi Jumatano, wakati ambapo hakimu
anatarajiwa kutoa hukumu yake dhidi ya Jolly.
Huenda akafungwa jela miaka 15 au kutozwa faini ya dola
mianne au adhabu zote mbili.chanzo BBC
No comments:
Post a Comment