Kamanda wa Polisi Mkoa Kigoma, Jafari Mohamed
WATU saba wanahofiwa kufa maji na wengine 49 wameokolewa
kutokana baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kukumbwa na dhoruba katika eneo
la vijiji vya mwambao wa kusini wa Ziwa Tanganyika.
Kamanda wa Polisi Mkoa Kigoma, Jafari Mohamed amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa boti ya mizigo ambayo ilikuwa imebeba
watu zaidi ya 50 ilikuwa ikitokea mkoani Rukwa kuelekea nchini Burundi.
wanahofiwa kufa
wakati polisi ikieleza kuwepo na taarifa za kifo cha mtu mmoja.
Kamanda Jafari alisema kuwa boti hiyo ilikumbwa na dhoruba
kati ya vijiji vya Sigunga na Herembe ambapo majira ya kati ya saa nane usiku
na saa kumi alfajiri kuamkia jana.
Alisema kabla ya kukumbwa na dhoruba na kuzama abiria
wakisaidiana na wafanyakazi wa boti hiyo walijaribu kutosa majini mizigo
mbalimbali iliyokuwemo kwenye boti hiyo lakini jitihada hizo hazikuzaa matunda.
Kamanda huyo wa polisi mkoa Kigoma alisema upo uwezekano wa
kuwepo kwa vifo zaidi katika tukio hilo na tayari vikosi mbalimbali vya ukoaji
vikihusisha polisi wanamaji, kikosi cha JWTZ cha wanamaji, SUMATRA na vikosi
vya ulinzi na usalama vimeelekea eneo la tukio.
Alibainisha kuwa juhudi za boti za wavuvi waliokuwa kwenye
shughuli zao za uvuvi zilisaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na hali ya
uokoaji na kuweza kufanikisha kuokolewa kwa watu hao 49.
No comments:
Post a Comment