Baba mmoja amejiua baada ya kuona picha za uchi zamwanawe wa
kike katika jarida la Playboy nchini Romania.
Loredana Chivu alirarua ukurasa uliokuwa na picha yake akiwa
'amepos' katika jarida hilo la Playboy na punde babake alipogundua kuhusu picha
hizo, alizongwa na mawazo na hata kumkana mwanawe.
Kwa mujibu wa mtandao wa Mirror, msichana huyo mwenye umbo
la kuvutia alisema, '' babangu aliacha kuongea na mimi na kuonekana mwenye
hasira sana''.
"alipogundua kuwa picha hizo zilikua zangu, alijitenga
sana na kujaribu kunitenga na mimi''.
Nilidhani labda angesahau na sikudhani hata siku moja
angejitoa uhai.
Loredana Chivu anasema anajuta sana kwani babake hakuwahi
kuongea naye baada ya kupata picha zake
Mwanamitindo huyo Loredana Chivu mwenye mamia ya picha akiwa
nusu uchi kwenye akaunti yake ya Instagram, alikuwa na uhusiano wa karibu sana
na babake lakini alisema yote hayo yalibadilika baada ya babake kuona picha
zake akiwa nusu uchi.
Alipokwenda kumtembelea babake miezi michache baadaye, baada
ya kuamua kwamba kimya kilikuwa kimeendelea kwa muda mrefu sana, alishtuka sana
kumpata babake akiwa amejitoa uhai
"nilipata akiwa na kamba shingoni akiwa ananing'inia
chumbani''.
Loredana,anayeishi nchini Romania, anasema kuwa tangu kifo
cha babake, amekuwa akiwaza na kuwazua kwamba aliamua kujiua kwa sababu ya
mgogoro kati yetu na hasa kuhusu picha zangu zilizoziona kwenye jarida la
Playboy.
''Najuta sana kwamba hakuwahi kupata muda wa kuzungumza na
babangu kuhusu yaliyotokea''.
''Hakuwacha ujumbe wowote kabla ya kujitoa uhai, siku zote
tulikuwa na uhusiano mzuri lakini yote yalibadilika baada ya baba kuona picha
zangu nikiwa uchi. Bado inaniuma sana na singemtakia mtu yeyote kupatwa na kama
yaliyonikuta''.
No comments:
Post a Comment