UKISTAAJABU ya Musa utayaona ya Firahuni! Binti
aliyefahamika kwa jina moja la Afsa (14), anayesoma darasa la 7, ametiwa
nguvuni na jeshi la polisi akidaiwa kuwafanyia ukatili na kuwadhalilisha watoto
wawili wa kiume (majina kapuni) wa mama yake mkubwa kwa kuwakang’ata nyeti zao
akiwalazimisha kufanya nao mapenzi.
Binti anayefahamika kwa jina moja la Afsa (14) anayetuhumiwa
kuwanyanyasa watoto wadogo.
Kamanda wa OFM, Mkoa wa Morogoro akiwa kazini, alipokea
taarifa kutoka kwa wananchi wa mtaa huo wakimuomba afike fasta.
Bila kuchelewa kamanda alitia timu na kukutana na akina mama
wawili ambao walishusha ‘vesi’ za tukio hilo:
Binti huyo akiwa chini ya ulinzi, wa pili kulia ni mmoja wa
watoto walionyanyaswa na binti huyo.
“Cha kushangaza Afsa amekuwa akiwafanyia ukaliti wa kutisha
watoto hao. Leo amewatoboa macho na njiti ya viberiti kuwapiga mateke na
kuwasukumiza ukutani, mbaya zaidi aliwang’ata nyeti zao alipokuwa
akiwalazimisha kuduu nao.
Makamanda wa Polisi wakimchukua mtoto mwingine
aliyenyanyaswa na binti mtuhumiwa.
Binti anayetuhumiwa akichukuliwa kwenye pikipiki kwenda
kituo cha Polisi.
“Mimi ni mfanyakazi pia mwanafunzi, nasoma chuo hivyo
wanangu hulelewa na Afsa ambaye ni mtoto wa mdogo wangu. Kweli wanangu
wamepigwa na kufanyiwa ukatili na huyu mtoto wa mdogo wangu lakini suala hili
sitaki lifike popote, nimepanga kumrudisha kwao Moshi,” alisema Mama Mese.
Katika hali ya kushanga, paparazi wetu alipotaka kumhojia
Afsa, mama huyo alikataa jambo lililowakera majirani na kuibua vurugu.
Baada ya vurugu kuwa kubwa, jirani mmoja aliwatonya polisi
ambao walifika ndani ya muda mfupi na kufanikiwa kumkamata Afsa kumpeleka
kituoni kwa ajili ya hatua za kisheria huku mjumbe wa serikali ya mtaa huo,
Yusuf Juma akishuhudia tukio hilo na kulilaani.chanzo GPL
No comments:
Post a Comment