Lori maalumu la usafishaji likiondoa theluji iliondoka
barabara ya South Church Street, katika mji wa Hazleton, Pennsylvania siku ya
Jumatatu Jan 26, 2015. Photo via dailymail
By Abou Shatry Washington DC
Zaidi ya watu 60 million wataadhithika kutokana na kimbunga
kikubwa cha upepo unaoambatana na unyeshaji wa theleji katika eneo la kaskazini
mashariki ya Marekani.
Kwa mujibu wa kitengo cha hali ya hewa nchini Marekani,
imetaja maeneo ambayo yataathiriwa na
tharuba hiyo, ya kihistoria ambayo
itapelekea zaidi ya watu kadhaa kukosa huduma ya umeme, pamoja na huduma za
usafiri wa anga na nchi kavu.
Imetaja baadhi ya majimbo ambayo yatakumbwa na kimbunga
hicho kuwa ni New York, New Jersey, Massachusetts, Connecticut na Rhode Island,
ambapo viongozi wakuu wamajimbo hayo kutangaza hali ya hatari kwa tukio hilo
ambalo litatokea siku ya Jumatatu, Jumanne na Jumatano.
Imetabiriwa kiasi cha unyeshaji wa theluji hiyo 36inches
katika jimbo la New York 16 hadi 26 inches katika jimbo la Boston, na kiwango
chengine kama hicho katika baadhi ya majimbo mengine.
Zaidi ya safari za ndege 3,800 zimesimamishwa mapema leo
Jumaatatu katia viwavya vya ndege vya JFK, LaGuardia na Newark airports, pia
huduma za shule kufungwa siku ya jumanne na jumatano katika majimbo hayo.
No comments:
Post a Comment