Tamko hilo limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mohamed Aboud Mohamed alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi katika Kongamano lililofanyika Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Fidel Castro na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, huko Pemba.
Alisema kwamba maamuzi hayo yamelazimika kufanyika baada ya kufanyika tathimini na kuona Dk Shein ameonyesha mwelekeo mzuri wa kisiasa na kiuchumi katika kipindi cha uongozi wake kutokana na utekelezaji mzuri wa Ilani ya uchaguzi baada ya kushika wadhifa huo mwaka 2010.
“Kamati maalum ya Halmashauri Kuu Zanzibar tumepitisha makubaliano na kumuomba aongeze kipindi kingine cha kugombea Urais kwa sababu ametekeleza vizuri ilani ya uchaguzi, sasa imebakia hiyari yake.”alisema Aboud ambaye Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa ya Cama hicho.
Aidha alisema kwamba katika kipindi chake Dk Shein ameonyesha uwezo, busara na hekima kubwa katika kuiongoza Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) na kufikia malengo ya kuanzishwa kwake ikiwemo kuondoa siasa za chuki na kujenga misingi ya umoja wa kitaifa kwa wananchi wake.
“Wakati ukifika tumekubaliana katika Kamati Maalum Dk Shein achukuwe fomu ya kugombea nafasi ya Urais wa Zanzibar.”alisema Aboud na kuibua shangwe kwa washiriki wa Kongamano hilo.
Mwaka 2005 Makamo wa Rais Muungano Dk Mohamed Bilal alijitokeza kuchukua fomu na kuchuana na Rais mstaafu Amani Abeid Karume na kuibua hekaheka kubwa ya kisiasa kabla ya kuombwa kuondoa jina lake na wazee kwa madhumuni ya kulinda umoja katika kuelekea Uchaguzi Mkuu.
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment