Facebook yapotea kwa dakika 40
Mtandao wa kijamii wa facebook ulikuwa hauingiliki katika
maeneo mengi duniani mapema leo kabla ya huduma zake kurudi.
Mamilioni ya watumizi wa mtandao wa facebook walishindwa
kuingia katika akaunti zao.
Wateja wake katika mataifa mengine walishindwa hata kutumia
hudumu ya Instagram.
Facebook ilisema kuwa wahandisi wake ndio walioababisha
tatizo hilo, na kukana madai kwamba kundi moja linalotekeleza uhalifu wa
mitandaoni lilihusika.
''Awali watu wengi walikuwa hawawezi kuingia katika
akaunti
zao za mitandao ya facebook pamoja na huduma ya Instagram'', msemaji wa
facebook aliiambia BBC.
''Hili halikuwa shambulizi kutoka kwa watu wengine lakini
lilitokea baada ya kufanya mabadiliko ambayo yaliathiri mpangilio wa mfumo
wetu''.
Tuliharakisha na kutatua tatizo hilo na sasa huduma zote
zimerejelea asilimia 100 kama kawaida
Mitandao hiyo ilitoweka kwa takriban dakika 40 kabla ya
kurudi.
Programu ya mtandao unaowaunganisha wapendanao Tinder ambayo
hutegemea facebook ili kutoa huduma zake pia iliathiriwa na tataizo hilo.
Kundi moja la uhalifu wa mitandano kwa jina Lizard Squad
liliandika ujumbe kwa twitter kuhusu hudumu hiyo kutoweka na kusababisha ripoti
kwamba huenda lilihusika.
Kundi hilo limeshtumiwa kwa mashambulizi ya mitandaoni
mwishoni mwa mwaka uliopita ambapo michezo ya video ya Sony pamoja na Xbox
ilipotea
No comments:
Post a Comment