Nakala Milioni za gazeti hilo zimeanza kusambazwa na
nyingine zitafuata iwapo wanunuzi wataongezeka.
Picha ya kibonzo hicho iliyopo ukurasa mbele wa gazeti hilo
inamwonyesha Mtume Mohammad akilia.
Wandishi wa jarida la Charlie Hebdo wamechapisha tena picha
ya kibonzo cha mtume Muhammad
Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa picha hiyo itachochea
chuki.
Hata hivyo waandishi wa habari wa gazeti hilo wanasema
ukurasa wa mbele unamaanisha Waandishi wa habari wamewasamehe waliotekeleza
shambulizi la kigaidi lilolofanyika jumatano wiki iliyopita.
Naibu Mhariri wa Gazeti la Liberalation Alexandra
Schwatzbrod anasema ulikuwa uamuzi mwepesi kwa gazeti lake kuchapisha picha ya
kibonzo hicho..
No comments:
Post a Comment