Real Madrid, mabingwa mara kumi wa Ulaya, wameweza
kushikilia nafasi ya kwanza kama timu tajiri zaidi duniani kwa mwaka wa kumi
mfululizo, katika orodha ya Deloitte ya timu tajiri duniani.
Manchester United imesogea hadi nafasi ya pili kutoka ya
nne, katika tathmini iliyofanywa kwa kuzingatia mapato ya msimu wa 2013-14.
Bayern Munich, Barcelona na Paris Saint-Germain zimechukua
nafasi ya tatu, nne na tano.
Klabu za England za Manchester City, Chelsea, Arsenal na
Liverpool zimo katika nafasi kuanzia sita hadi tisa, zote zikionesha ongezeko
zuri la mapato.
Orodha kamili ya kumi bora pamoja na mapato msimu wa 2013-14
ni kama ifuatavyo kwa sarafu ya Euro:
(Kwenye mabano ni mapato ya msimu wa 2012-13)
•1. Real Madrid: 549.5m (518.9m)
• 2. Man Utd: 518m (423.8m)
• 3. Bayern Munich: 487.5m (431.2m)
• 4. Barcelona: 484.6m (482.6m)
• 5. Paris Saint Germain; 474.2m (398.8m)
• 6. Manchester City: 414.4m (316.2m)
• 7. Chelsea: 387.9m (303.4m)
• 8. Arsenal: 359.3m (284.3)
• 9. Liverpool: 305.9m (240.6m)
• 10. Juventus: 279.4m (272.4m)
No comments:
Post a Comment