Kiungulia
Madaktari mjini Devon wanaunga mkono kampeni mpya
inayowaagiza raia kuwatembelea madaktari wao iwapo wanahisi kuwa na kiungulia
kwa siku kadhaa kwa kuwa huenda ikawa ishara ya ugonjwa wa saratani.
Zaidi ya watu 10,000 hufariki kutokana na saratani ya tumbo
ama ile ya koromeo kila mwaka nchini
Uingereza ambayo ni sawa na watu 28 kila
siku.
kampeni hiyo inayofanywa na idara ya afya ya uma nchini
Uingereza inasema watu sita kati ya kumi hawajui kwamba kiungulia huenda kikawa
ishara ya Saratani.
Pia inasema kuwa karibia nusu ya watu hutembelea madaktari
wao iwapo wanaugua kiungulia kwa wiki tatu ama zaidi.
Daktari Tom Debenham kutoka Devon na mkuu wa kliniki za
kazkazini,mashariki na magharibi mwa Devon anasema kuwa watu wanafaa kuelezwa
kuhusu uhusiano kati ya kiungulia na saratani.
''Iwapo unahisi kiungulia kila mara,nenda ukamuone daktari
,hata iwapo unatumia dawa na unahisi zinakusaidia''.
''Huenda si kitu chochote hatari lakini iwapo ni saratani
kuigundua mapema inakuwa rahisi kuitibu.'',alisema daktari huyo.
Watu pia wameagizwa kuwatembelea madaktari wao iwapo kila
wanapomeza chakula wanahisi kwamba chakula kinazuiliwa katika koromeo.
No comments:
Post a Comment