Libby Lane kuwa kasisi wa kwanza mwanamke
Kanisa moja nchini Uingereza jana limemuapisha mwanamke
wa kwanza kuwa kasisi.
Mchungaji Libby Lane kama anavyojulikana sasa atakuwa kasisi
wa Stockport katika sherehe iliofanyika katika eneo la York Minster,ikiwa ni
miezi sita tu baada ya kanisa hilo kumpigia kura ili kumaliza utamaduni wake wa
wanaume kuwa makasisi.
Kasisi huyo amesema kuwa iwapo uchaguzi wake utawafanya
wanawake kubaini uwezo wao basi anafurahia.
Hatua hiyo imeendelea kuzua hisia tofauti miongoni mwa
wafuasi wa kanisa hilo la kianglikana duniani.chanzo BBC
No comments:
Post a Comment