Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, January 5, 2015

MAKALA: WATANZANIA TUNAJIFUNZA NINI KUTOKA KWA MTOTO KELVIN DOE RAIA WA SIERRA LEONE



Kelvin Doe alizaliwa Freetown, Sierra Leone mnamo mwaka 1996 akiwa ni mtoto wa mwisho kati ya watoto watano wa familiya yao. Amekuwa na kipaji cha ubunifu tangu angali mdogo; mara kwa mara aliwazia masuluhusho ya utatuzi wa masuala mbali mbali yaliyoikabili jamii yake. Katika umri wa miaka 10, alianza kuchakura chakura skrepa za vyombo vya kielektroniki katika majalala kila alipotoka shule ili afanye uvumbuzi wake.
Kelvin, pamoja na timu yake, walikuwa washindi wa Global Minimum’s Innovate Salone 2012 tuzo ya changamoto za ubunifu katika shule za sekondari nchini Sierra Leone. Ameunda kituo cha redio kwa kutumia skrepa anazookota kwa jamii yake, aidha, ameunda betri na jenerata. Kelving alichaguliwa kwenda Marekani mwaka 2012, alikuwa mwalikwa mnenaji katika jopo la Vijana Waundaji ( Meet the Young Makers panel ) kwa World Maker Faire 2012 katika jiji la New York. 




Kelvin, rasmi alikuwa ndiye mtaalam mwalikwa kijana mdogo katika Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts (MIT). Pale MIT aliwasilisha uvumbuzi wake kwa wanafunzi wa maabara za D, na kwa jumuiya ya MIT; aidha, alishiriki kwenye utafiti mdogo katika maabara za Upashanaji Habari za MIT. Pia, alitoa mhadhara kwa wanafunzi wa shahada ya kwanza ya injinia katika chuo cha Harvard.

YouTube video inayoonesha uzoefu wa Kelvin imeshatazamwa zaidi ya mara milioni 4 na bado inavutia vijana wengi nchini mwake na ulimwenguni kwa jumla. Kwa sasa Kelvin angali anaendelea na masomo yake ya elimu ya sekondari katika shule ya Prince of Wales nchini Sierra Leone.
“ Ninaamini kwamba kupitia uvumbuzi, tunaweza kulijenga taifa letu Sierra Leone.” – Kelvin Doe.
Tazama hapa video yake


CHANZO: AMAZING STUFF

No comments:

Post a Comment