Mtoto mchanga mwenye umri wa mwezi mmoja, Yadiko Chigoda
amelazwa katika Hospital ya Benjamini Mkapa Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma
baada ya kupigwa na mchi kichwani na baba yake mzazi na kumsababishia maumivu
makali.
Amesema katika ugomvi huo walikuwa wanapigana na fimbo,
hivyo alipowanyang’anya fimbo hiyo ili wasiendelee kupigana ndipo (Chigoda)
alipoamua kuchukua mchi ili ampige nao mkewe kichwani lakini alikwepa na
alipourusha ndipo ulipompata mtoto huyo kichwani.
“Nilipowanyang’anya fimbo ili wasiendelee kupigana, mume
wangu aliokota mchi na kunirushia kichwani.. kwa bahati nzuri niliuona mchi huo
na kukwepa ili usinipige ndipo ulipompiga kichwani mwanangu niliyekuwa
nimembeba mgongoni,” amesema Carolina.
Ameongeza kuwa, “Baada ya kuona kuwa amempiga mtoto
alikimbia na hajulikani alipo mpaka sasa.”
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Said Mawji amethibitisha
kumpokea mtoto huyo na kwamba hivi sasa mtoto huyo anaendelea kupata tiba na
uchunguzi zaidi wa afya yake.
“Ameumia sana kichwani lakini bado tunampatia tiba na
uchunguzi zaidi kwenye fuvu la kichwa, kwani inaonekana kama vile limepasuka,”
amesema Dk, Mawaji.
Hata hivyo amesema kuwa wanafanya mpango wa kumpa rufaa
mtoto huyo ili aweze kwenda kutibiwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Dodoma.
Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Mingui, Mwingwa Udoba amesema
chanzo cha tukio hilo ni ugomvi wa kifamilia na kwamba bado wanamtafuta baba
mzazi wa mtoto huyo kwa kuwa alikimbia baada ya tukio hilo.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime alipotafutwa
kuzungumzia tukio hilo simu yake ilipokelewa na mtu aliyesema kuwa Kamanda
alikuwa kwenye kikao cha kazi.
No comments:
Post a Comment