Muhubiri wa kiislamu Abu Hamza aliyepewa kifungo cha maisha
Mhubiri wa kiislamu Abu Hamza amehukumiwa kifungo cha maisha
gerezani kwa makosa ya ugaidi katika mahakama moja mjini New York.
Mhubiri huyo alifukuzwa nchini Uingereza mwaka 2012 kufuatia
kesi ya muda mrefu na alipatikana na hatia miezi minne iliyopita.
Alipatikana na hatia katika mashtaka kadhaa ikiwemo njama ya
kuwateka nyara watu kutoka nchi za
magharibi ikiwemo Yemen mwaka 1998 na
majaribio ya kuanzisha kituo cha mafunzo ya ugaidi kwenye jimbo la Oregon
nchini Marekani.
Jaji alisema kuwa Abu Hamza alikuwa amewachochea watu
wengine kuwaua wale wasio waislamu kama jukumu la kidini na kusema kuwa alikuwa
hatari kwa jamii.
Alifahamika kwa kutoa hotuba kali kwenye msikiti mmoja mjini
London.
No comments:
Post a Comment