Mwanablogu wa saudi Arabia aliyehukumiwa kifungo cha 10
Mwanablogu nchini Saudia amechapwa viboko hadharani kwa
madai ya kutusi dini ya kiislamu.
Raif Badawi ambaye alianzisha mtandao kwa jina ''Liberal
Saudi Network'' alihukumiwa kifungo cha miaka 10 msimu wa joto uliopita.
Mahakama pia iliagiza acharazwe viboko 1000.
Amechapwa viboko hivyo katika mji wa Jeddah.
Ilieleweka kwamba angetandikwa viboko hamsini na kwamba
alitarajiwa kuchapwa viboko zaidi wiki
zilizofuatia.
Mwanablogu huyo alichapwa viboko licha ya wizara ya maswala
ya kigeni nchini Marekani kutaka kuondolewa kwa adhabu hiyo walioitaja kama ya
kikatili.
No comments:
Post a Comment