Tukio hilo ambalo limeishangaza nchi hasa kufanywa na mama
mzazi ambaye anaujua uchungu wa kuzaa, lilijiri Jumapili usiku ndani ndani ya
nyumba ya mwanamke huyo.
SIKU MOJA KABLA
Taarifa kutoka vyanzo vya uhakika, siku moja kabla ya tukio,
mwanamke huyo ambaye ni mtata kiasili alionekana akicheza na watoto wake na
watoto wa jirani huku akionesha uchangamfu mkubwa.
“Kama wale watoto wake wangejua mama yao mzazi ndiyo safari
ya kifo chao naamini wasingemchangamkia mama yao.
“Walicheza kwa amani, kwa upendo. Kumbe mama ana mahesabu
yake. Haiwezekani leo niambiwe kuwa mawazo ya kuwaua watoto wake aliyapata
ghafla,” alisema shuhuda mmoja.
Mtuhumiwa akiwa chini ya ulinzi.
USIKU, JIRANI ASIKIA KISHINDO
Jirani mmoja na nyumba ilipotokea tukio alisema:
“Mimi awali ya siku ya kuelekea usiku wa tukio, nilimwona
yule mama. Nikasalimiana naye. Alionekana yupo kawaida tu.
“Lakini usiku, kukiwa kumetulia nilisikia vishindo kama mtu
anachimba ardhi. Nilipofuatilia nikabaini vilikuwa vikitoka upande wa nyumbani
kwa mwanamke yule.“Sikushtuka. Nilijua ni shughuli zake za kawaida zinaendelea ndani ya nyumba yake.
Kulipokucha sasa, nikasikia yule mama anasema kwamba watoto wake wamepotea.
“Palepale nikaanza kuhisi kitu kwa ile mishindo ya usiku.
Inaonekana alishawaua watoto wake sasa alikuwa anachimba mashimo ya kuwafukia.
Kule si kuwazika na yale si makaburi ni mashimo.
“Inauma sana, siamini kama mama aliyezaa watoto kwa uchungu
mkubwa anaweza kufanya ukatili kama huu.”
Miili ya watoto hao baada ya kufukuliwa kwenye mashimo.
AKILI ILIMWAMBIA ASUBIRI AKIWA PEKE YAKE
Baadhi ya majirani walisema ndani ya nyumba hiyo kuna watu
wengine wanaishi, lakini mtuhumiwa huyo alisubiri akiwa peke yake ndipo
akatekeleza ukatili wake wa kutisha.
ANACHOJUA MWENYEKITI WA MTAA
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Utusi, Aziza Mwenya, ushirikiano mkubwa kati ya
wananchi wa mtaa huo
ndiyo uliofanikisha kugundulika kwa tukio
hilo la kinyama
lililopoteza maisha ya
watoto hao wasiokuwa na hatia.
“Baada ya kupokea taarifa kutoka
kwa babu wa
Zuhura, mzee Shaban Ramadhan kuhusu
kutoweka kwa watoto hao katika
mazingira ya kutatanisha, tulifika
kwenye nyumba ya tukio kwanza na kumhoji
mama wa watoto.
Ndugu na majirani wakiwa na makamanda wa Polisi eneo la
tukio.
“Cha ajabu alikuwa
akizuia watu kuingia ndani. Kumbe alishajua
kinachoendelea na akiruhusu sisi kuingia nini kitatokea.“Hata hivyo majirani
kwa kushirikiana na mimi na baba wa mmoja wa watoto waliouawa (Sudi Mrisho),
Mrisho Abdallah tulimshika kwa nguvu
Zuhura, watu wakaingia.”
WAKUTA MASHIMO MAWILI
“Tulipofika, tukabaini mashimo mawili aliyokuwa amewafukia
watoto wake. Shimo moja sebuleni, jingine chumbani. Tuliwapa taarifa polisi
wakafika haraka sana. Mashimo yalipofukuliwa, watoto walikutwa ndani ya mifuko
miwli ya sandarusi. Inauma sana. ”
MTUHUMIWA AZUNGUMZA NA AMANI
Amani lilibahatika kuzungumza na mwanamke huyo katika
mahojiano mafupi akiwa chumbani muda mfupi kabla ya polisi kufika.Amani: “Hivi
Zuhura, ni kwanini umeamua kuwaua watoto wako wa kuwazaa?”
Zuhura: “Nani? Mimi sijui, we (mwandishi) ndiyo
unajua.”Amani: “Watoto wako wako wapi?”
Zuhura: “Nani? Wako wapi kwani?”
KILICHOONEKANA
Baadhi ya wakazi wa eneo hilo walisema, Zuhura licha ya
kuonekana hana wasiwasi wowote, lakini pia aliashiria kujitoa ufahamu ili
atafsirike kwamba hakuwa na akili timamu.
KUMBUKUMBU MBAYA
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa majirani zinadai kuwa,
mwaka 2013, Zuhura alidaiwa kumsababishia kifo mtoto wake mchanga wa kiume kufuatia kumzidishia dozi ya malaria
wakati alipokuwa akiumwa.
KAMANDA WA POLISI
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Juma Bwire ilikiri kutokea kwa tukio
hilo.
Afande Bwire alisema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada
ya upelelezi kukamilika.CHANZO GPL
No comments:
Post a Comment