Fulana iliyozua utata
Rihannaameshinda kesi ya madai dhidi ya duka la mavzi la
Topshop juu ya fulana iliyobandikwa sura yake.
Duka hilo liko mtaa wa maduka yenye mavazi ghali nalo
limekata rufaa kutokana na maamuzi ya kuwa kuuza fulana zenye picha hiyo bila
makubaliano na mhusika ni kosa la jinai na hakuna haki miliki iliyowekwa dhidi
ya bidhaa hiyo.
Lakini katika kile kinachoonekana kama maamuzi muhimu
ilibidi yachukuliwe kuzuia uuzwaji wa fulana hizo za kata mkono.
Wakili wa mwanamuziki huyo nguli wa miondoko ya POP anadai
kwamba picha inayoonekana katika
fulana hiyo haikuruhusiwa kutoka,na
ilichukuliwa wakati nyota huyo alikuwa akichukua picha za video huko Kaskazini
mwa Ireland kwa ajili ya wimbo wake ulioachiliwa mwaka 2011,na hivyo duka hilo
la Topshop linabaki na zuio hilo la kutokuwa na haki ya kuuza bidhaa hiyo.
Duka hilo kubwa lilijitetea kuwa limekuwa likichapisha sura
za wasanii miaka kadhaa iliyopita katika fulana na Rihanna si wa kwanza,wapo
waliotangulia kama Elvis Presley, Jimi Hendrix na Prince.
Kutokana na hali hiyo Geoffrey Hobbs wakili anayetetea duka
hilo anadai kuwa kuwazuia kutouza bidhaa hiyo ni matumizi mabaya ya sheria .
Bwana Hobbs ameongeza kwamba jamii haiamini kwamba kila sura
ya mtu maarufu unayoiona katika vazi basi imepewa ruhusa na mhusika,hata hivyo
Rihanna ameshafanya biashara na kupata faida kubwa na maduka makubwa ya mavazi
kama Topshop wenyewe na mpinzani wake River Island.
Hakuishia hapo katika kukosoa hukumu hiyo ya maahakama kuu kwamba
watu maarufu hawana mamlaka ya kuingilia kazi zao za uzalishaji na Topshop
walipoamua kutumia sura ya mwanamuziki huyo haina maana kuwa wamempitia tu lah.
Hukumu hiyo inadaiwa ilikuwa imeangazia na kulinda hadhi na
heshima ya msanii huyo asije akaharibiwa nia yake njema katika tasnia ya
mavazi.
No comments:
Post a Comment