Meli kubwa zaidi duniani imetia nanga nchini Uingereza kwa
mara ya kwanza wakati huu ikiendelea na safari yake duniani, je Meli hii ina
nguvu kiasi gani na ukubwa gani?
Meli iitwayo the Globe ina urefu wa mita 400 ikifananishwa
na ukubwa wa mabwawa manane yanayotumika katika michuano ya Olimpiki ina upana
wa mita 56.8 na upana wa mita 73 kwenda juu, ina uwezo wa kubeba mzigo wa tani
186,000.
Meli kubwa
Shuhuda wa Meli hiyo anasema ''ukiitazama meli hiyo
utajihisi mbilikimo ni Meli kubwa mno''.
Safari ya Meli hiyo ilianzia mjini Qingdao nchini China
tarehe 3 mwezi Desemba mwaka jana na inatarajiwa kumaliza ziara yake tarehe 25
Februari.
Hii ni meli ya kwanza kubwa zaidi kati ya meli kubwa
tano
zenye umbile kama Globe kutengenezwa Korea kusini, Meli zote zinatarajiwa
kutolewa ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
No comments:
Post a Comment