Pages

Wednesday, January 14, 2015

TETESI ZA SOKA ULAYA- DIRISHA DOGO LA USAJILI

Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi, 27, amewashtua Manchester United kutokana na kuashiria upatikanaji wake baada ya kusema hajui atachezea timu gani mwaka ujao (Guardian) Man Utd pia wanafikiria kumchukua kiungo wa Southampton Morgan Schneiderlin, 25 ili kuimarisha nguvu wakinyatia kucheza Champions League (Daily Express), pia United wanamfuatilia mshambuliaji wa Bayern Munich Thomas Muller, 25, ambaye anataka kuondoka Allianz Arena (Daily Star), Swansea City wanamtaka Papiss Cisse, 29 wa Newcastle kuziba pengo wa Wilfried Bony, 26 aliyekwenda Manchester City (Daily Telegraph), Liverpool wapo tayari kumuuza kiungo kutoka Brazil Lucas Leiva, 28, kwenda Napoli iwapo watampata Fabian Delph, 25, kutoka Aston Villa (Daily Mirror), 
Juventus wanataka kumchukua Mario Balotelli, 24, kwa mkopo na uwezekano wa kumsajili moja kwa moja kwa pauni milioni 14 mwisho wa msimu (Times), Arsenal wanajiandaa kuongeza dau ili kumpata kiungo Krystian Beilik, 17 kutoka Legia Warsaw ya Poland, lakini wanakabiliwa na upinzani kutoka Hamburg ya Ujerumani (Times), Arsenal pia wamekuwa 'wakimchombeza' mshambuliaji wa Swansea Bafetimbi Gomis, 29 (Daily Mail), kiungo wa West ham Ravel Morrison, 21, anakaribia kuhamia Lazio ya Italia baada ya kukosa namba Upton Park (Mirror), mshambuliaji wa Tottenham Emmanuel Adebayor anafanya mazungumzo na Parma ya Italia, lakini madai ya mshahara mkubwa


 huenda ikawa kikwazo (London Evening Standard), meneja wa Everton Roberto Martinez atatupilia mbali dau lolote kwa Seamus Coleman, 26 ambaye ananyatiwa na Manchester United (Sun), beki wa Real Madrid Alvaro Arbeloa, 31, huenda akakataa kujiunga na Arsenal na Chelsea na badala yake kurejea Liverpool (Daily Express). Katika habari nyingine meneja wa Manchester United Louis van Gaal amemuomba Zen Master - mtaalam wa ndondi kutoka Thailand- kuzungumza na kikosi chake ili waweze kujitazama kimawazo na kihisia (Sun). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Habari za uhamisho zilizothibitishwa, nitakujulisha zitakapothibitishwa. Shukran sana- kumradhi kwa tetesi kuchelewa. Na Salim Kikeke

No comments:

Post a Comment