Swansea City wamekubali ada ya uhamisho ya takriban pauni
milioni 30 kutoka kwa Manchester City ya kumnunua Wilfried Bony, 26.
Meneja wa Swansea, Gary Monk alisema kuwa itahitaji
"kitita cha ajabu" kumhamisha Bony kutoka Swansea.
Alikuwa mfungaji bora wa mwaka wa kalenda 2014 akipachika
mabao 20.
Bony alijiunga na Swansea mwaka 2013 akitokea Vitese Arnhem
kwa pauni milioni 12.
Mchezaji huyo alifunga bao la kusawazisha katika dakika ya
90 kwenye mechi dhidi ya QPR siku ya mwaka mpya.
Bony kwa sasa yuko na kikosi cha timu ya taifa ya Ivory
Coast kujiandaa na michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.
No comments:
Post a Comment