Mwili wa kitoto kichanga uliotupwa kwenye jalala.
Stori: Mwandishi Wetu, Mbeya/UWAZI UKATILI,
Mtoto mchanga ambaye anasadikika kuwa wa siku saba, amekutwa akiwa
ameuawa na mwili wake kuwekwa kwenye mfuko wa rambo kisha kutupwa
pembeni mwa jalala. Tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika Mtaa wa
Kaloleni katika Mji wa Tunduma katika Wilaya ya Momba, mkoani Mbeya .
Wakizungumza na gazeti hili mashuhuda ambao hawakupenda majina yao
kuandikwa gazetini walisema kuwa walimkuta mtoto huyo akiwa amenyongwa
kisha kuwekwa kwenye karatasi ya naironi (rambo) .
Waliongeza kuwa mtoto huyo alitambulika
baada ya watoto wadogo wakiwa katika michezo yao katika maeneo yao
kuuona mfuko huo wa rambo na kuufungua ndipo wakatoa taarifa wa wazazi
wao,” alisema mmoja wa wazazi wa eneo hilo.
Msemaji wa jeshi la Polisi mkoani Mbeya, SACP Ahmed Msangi.
“Hiki kitendo ni kibaya sana na aliyefanya unyama huu anastahili
adhabu kali. Huwezi kulea mimba miezi tisa kisha unamza mtoto na
kumnyonga shingo hadi kufa, ni ukatili uliokithiri, tena mtoto huyu ni
kama wa siku saba, hii ni kwa sababu kitovu chake kilionesha dalili za
kupona,” aliongeza.
Hata hivyo, aliyefanya kitendo hicho cha kikatili
hakuweza kutambulika mara moja.
Wakithibitisha habari hiyo, kiongozi mmoja wa polisi katika kituo kidogo cha Tunduma alisema ni kweli kimetokea na mwili huo wa mtoto huyo umepelekwa katika hospitali ya serikali iliyopo mjini hapa kwa ajili ya uchunguzi.
hakuweza kutambulika mara moja.
Wakithibitisha habari hiyo, kiongozi mmoja wa polisi katika kituo kidogo cha Tunduma alisema ni kweli kimetokea na mwili huo wa mtoto huyo umepelekwa katika hospitali ya serikali iliyopo mjini hapa kwa ajili ya uchunguzi.
“Tunaomba wenye kujua aliyefanya haya atuletee jina ili tumkamate,”
alisema ofisa huyo bila kutaja jina lake kwa kuwa siyo msemaji wa
polisi. Msemaji wa jeshi hilo mkoani Mbeya ni SACP Ahmed Msangi
(pichani).
No comments:
Post a Comment