Tabasamu la matumaini.
Mwanamume mmoja mwenye asili ya nchini Mali ambaye
aliwaficha wauza maduka katika duka kubwa maarufu kama supermarket mjini Paris
wakati wa shambulio la kigaidi lililotekelezwa na watu wanaodhaniwa wapiganaji
wa kiislamu amepewa hati halali ya ukaazi na kuwa raia halali wa Ufaransa.
Kwa pamoja waziri mkuu wa Ufaransa Manuel Valls na waziri wa
mambo ya ndani Bernard Cazeneuve walizungumza katika karamu ya kumpongeza na
kumshukuru Lassana Bathily kwa ushujaa wake kwa niaba ya taifa lake .
Kijana huyo ana umri wa miaka ishirini na minne, na kazi
aifanyayo ni muuzaji msaidizi katika supermarket hiyo,ambaye alifanya kazi
kubwa ya kuwaongoza na kuwaficha katika eneo la juu la
chumba baridi cha
kuhifadhia bidhaa na kisha akazima taa za duka hilo kubwa ,kisha akawapigia
polisi simu kwa msaada wakati walipovamiwa.
Baada ya tukio hilo, likapitishwa azimio aitwe apewe uraia
wa nchi hiyo ya Ufaransa ,hata hivyo inaelezwa kwamba Bathily ameishi nchini
humo kwa miaka tisa sasa na alikuwa ameshaomba ridhaa ya kuwa raia halali wa
nchi hiyo mwaka wa jana.
Wakati wa uvamizi huo, Amedy Coulibaly,aliwaua watu wane
wenye asili ya Uyahudi katika duka hilo kubwa kabla hajapigwa risasi na polisi
na kufa.CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment