Mtandao wa WjhatsApp
Mtandao wa kijamii wa WhatsApp unawabana watu wanaotumia
huduma hio kupitia programu bandia na ambayo haijaidhinishwa ya Android kwa
muda wa saa 24.
WhatsApp ambayo inamilikiwa na Facebook, ilisema kuwa
imechukua hatua dhidi ya watumiaji wa huduma ya WhatsApp Plus kwa sababu ya
wasiwasi kwamba programu hiiyo huenda iksababisha kuvuja kwa taarifa za siri za
watumiaji wa WhatsApp.
Programu hio bandia na isio rasmi ya Android inawezesha
watumiaji wa WhatsApp Plus kupamba mawasiliano yao wanavyotaka.
Wataalamu wanasema kwamba watumiaji wa Android wanapaswa
kuwa makini na kutahadhari kuhusu wanavyodownload programu flani au 'Apps'.
Mtandao wa WhatsApp ulisema hivi karibuni kwamba ina
watumiaji milioni 700 wanaotuma ujumbe bilioni 30 kila siku. Kwa sasa inatoza
dola 0.99 kwa watumiaji wake wanaotumia huduma ya WhatsApp Plus kila mwaka.
''Lengo letu ni kuhakikisha kwamba huduma ya WhatsApp ni ya
kasi kwa wanaoitumia, hilo ndio jambo muhimu sana kwetu,'' alisema msemaji wa
kampuni hio.
''Watu wengine wamebuni progarmu ambazo bado
hazijaidhinishwa na sasa wanazitumia na WhatsApp , kitu ambacho kinaweza
kusababisha kupotea kwa ujumbe au baadhi ya taarifa kuvujishwa. ''
''Bila shaka jambo hili linakwenda kinyume na malengo yetu
ya kutoa huduma kwa wateja wetu. Kuanzia leo tutaanza kuchukua hatua kali dhidi
ya wanaotumia programu ambazo hazijaithinishwa ili kuweza kutumia programu zetu
na pia kuwatahadharisha wanaozitumia programu hizo''.
Kulingana na moja ya maduka ya kuuza programu za kwenye
mitandao, programu ya WhatsApp Plus yenyewe ilikuwa imekuwa dowloaded mara
milioni 35
No comments:
Post a Comment