Miezi minne iliyopita, Demeteriya Nabire aliliwa na mamba
alipokwenda mtoni karibu na makazi yake kuchota maji. Mnyama huyu alirudi tena
baaae katika eneo lilelile na kumkuta mume wa Nabire anasubiri, tayari kwa
kulipa kisasi.
Demeteriya Nabire alikuwa kwenye kingo za mto akiwa na
wanawake wengine kutoka kwenye Kijiji anachoishi, walikuwa wakichota maji
kutoka katika Mto Kyoga nchini Uganda, Mamba alifika na kumnyaka.alimburuza
kisha mwanamama huyu hakuonekana tena.
Mumewe, Mubarak Batambuze, aliingiwa na hofu sana,Nabire
alikuwa mjamzito.hivyo Mubarak hakupoteza mkewe tu bali kiumbe kilichokuwa
tumboni.alijihisi kukosa nguvu, lakini Mwezi uliopita akasikia kuwa Mamba
amerejea.
''Mtu mmoja akaniita 'mubarak nina habari kwa ajili yako,
Mamba aliyemchukua mkeo amerudi, tena'
Mvuvi huyo mwenye umri wa miaka 50 akaelekea mtoni na
marafiki zake .''alikuwa mkubwa, na
tulijaribu kupambana nae kwa mawe na fimbo
lakini hatukufanikiwa''.alisema.
Hivyo Batambuze alienda nyumbani kwa muhunzi.
''nikamweleza kuwa napambana na Mamba ambaye amenichukulia
mke wangu na mtoto aliyekuwa tumboni.ninataka sana kulipa kisasi,kisha
nikamwambia anitengenezee silaha ambayo ingeweza kumuua mamba huyo.
Mtu huyo alitaka nilipe kiasi cha pauni 3.20 ili atengeneze
Mkuki.
Akiwa na mkuki wake mkononi alielekea kwenye mapambano.
Lakini alipofika kwenye maji, Mamba alikuwepo eneo hilo,
lakini Marafiki wa Batambuze waliingiwa hofu na kumsihi asimshambulie kwa kuwa
alionekana mkubwa sana na angeweza kumla,wakamwambia kuwa Mkuki huo hautafaa.
Batambuze akasisitiza waendelee kubaki, ''nilishindwa kumuua
mwanzo, alisema, ''sioni tatizo nikifa wakati namuua Mamba natatumia mkuki huu,
na nitahakikisha amekufa''.
Ofisa wa wanyama pori Oswald Tumanya, amesema kuwa Mamba
alikuwa na urefu wa zaidi ya mita nne na uzito wa kilo 600.
Mubarak Batambuze akimshuhudia mamba aliyemuua mkewe
''nilikuwa na wasiwasi sana lakini kilichonisaidia ni
Mkuki''alisema Batambuze.
Alifunga kamba kwenye kwenye mkuki kwenye sehemu
iliyotengenezwa mithili ya kisu kikali, ''niliweka silaha yangu eneo Mamba
alipo huku marafiki zangu wakinisaidia kurusha mawe na kumchapa mamba mgongoni
kwake wakitumia fimbo, Alijaribu kunyanyua mdomo wake juu ili anishambulie.''
alishikwa na hasira sana, kisha kulikuwa na hofu sana katika
eneo hilo, lakini nilikuwa na nia, na sikuhofu kufa, nilitaka kumuua hivyo
nilirusha silaha yangu alipo mamba kisha nikavuta kamba. Mamba alianza kuwa
matatani''.
Ilichukua saa moja na nusu mwa Batambuze na marafiki
zake,wakipambana na Mamba, hatimaye alikufa.
Wakiwa wamechoka walirejea kijijini kwao ''kulikuwa na
mshtuko mkubwa, kilichomshangaza kila mtu ni ukubwa wa Mamba, hakuwa mamba wa
kawaida, alikuwa mkubwa sana .Na Watu wakatuita mimi na marafiki zangu
mashujaa''alisema.
No comments:
Post a Comment