Baada ya kuwa na ndoto za kuendesha gari ya kifahari aina ya
Lamborghin huku akiwa hana uwezo wa kununua gari hiyo Yu Jietao raia wa Jiangx,
China amewashangaza watu wengi baada ya kuja na staili yake ya kutengeneze gari
kama hiyo ili atimize ndoto zake.
Jamaa huyo alifikia uamuazi wa kutumia mbao na kutengeneza
gari yenye muundo wa Lamborghin
baada ya kuona hana uwezo wa kumudu gharama za gari hilo zinzofikia Euro 260,000 hivyo akaamua kufanya hivyo ili kulinganisha na gari hiyo yenye thamani.
baada ya kuona hana uwezo wa kumudu gharama za gari hilo zinzofikia Euro 260,000 hivyo akaamua kufanya hivyo ili kulinganisha na gari hiyo yenye thamani.
Kwa kutumia taaluma yake ya ufundi seremala Jietao aliamua
kutafuta mbao na kutengeneza gari lenye kufanana kabisa na gari hiyo huku
akiweka vifaa vingine vyote vinavyowezesha gari hiyo kutembea na kufanya kazi
kama kawaida.
Muenekano wa gari hiyo umekua kivutio kikubwa kwa watu wengi
huku wakijaribu kutaka kulinunua kwa gharama kubwa lakini mwenyewe amesema
hawezi kuliuza.
No comments:
Post a Comment