Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 (wa pili kulia) akiongoza vijana wake kutoa burudani kwa mashabiki wa bendi hiyo Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar. Kutoka kushoto ni mwimbaji Baby, Ashura Kitenge pamoja na Sam Mapenzi.
Ijumaa hii Skylight Band hawatopiga Thai Village watakua njiani wakitokea nchini Oman, wanaomba radhi kwa usumubufu wowote utakaojitokeza kwa wateja wao.
Ila siku ya Jumamosi siku ya wapendanao (Valentine's Day) Skylight Band wataporomosha burudani ya nguvu na ya aina yake kwa mashabiki wao ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar huku mashabiki wakipata fursa ya kuchagua nyimbo wazipendazo zinazoendana na siku hiyo maalum pamoja na kugawa zawadi kwa "couples" itakayonoga na kutokelezea.
I'm Going Koo Koo Koo, So Koo Koo Coz I, I, Love You, (Aiyayaaaaa)...I'm Going Koo Koo Koo, So Koo Koo Coz I, I Love You,.....(Aiyayaaaaa)...Mmm Take Me,....Nitembee Nawe,.....Baby Take Me, Nitembee Nawe....Aneth Kushaba AK47 akipiga kolabo na Sam Mapenzi
Kikosi kazi cha Skylight Band wakisakata lisebene.
Moja ya zawadi ndani ya usiku maalum wa Valentine's ni hii Membership card aliyoshika mdau Francis Machibya, ambayo inakupa nafasi ya kuhudhuria show zote za Skylight Band zinazofanyika Thai Village bure kwa mwaka mzima.
Mashabiki wa Skylight Band wakicheza moja ya style inayofahamika kama "Yachuma chuma".
Sehemu ya umati wa mashabiki wa Skylight Band wakisebeneka.
Ashura Kitenge akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) huku akipewa sapoti na Aneth Kushaba AK47 pamoja na Baby.
Wadau wakinywa na ku-enjoy muziki mzuri wa Skylight Band.
Sam Mapenzi akikonga nyoyo za mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita huku akipewa sapoti na John Music pamoja na Sony Masamba....Usikikose Jumamosi hii Valentine's day Thai Village watakinukisha.
Sam Mapenzi akiongoza mashabiki wa Skylight Band kwa style ya aina yake.
Sony Masamba akijimwaga na shabiki wake kwenye dancing floor.
Katika kupika mziki mzuri wa Skylight Band ukanoga basi huyu jamaa James Kibosho, anahusika sana na hivi sasa ametua Skylight Band.
Kiungo kingine chenye vipaji lukuki si mwingine ni Danny Kinanda akifanya yake.
Burudani ikiendelea.
Pale mzuka wa mashabiki unapopanda.
Kwa matukio mnegi zaidi ingia hapa
No comments:
Post a Comment