BABA mzazi wa msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya hapa
nchini, Dully Sykes, mzee Ebby Sykes amefariki dunia jioni ya leo katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu
ya ugonjwa wa Presha.
Ebby Sykes alikuwa muimbaji na mpiga gitaa mashuhuri na
ndiye anayedaiwa kumfundisha mambo mengi ya muziki mwanae Dully Sykes.
Sykes alizaliwa February 24, 1952 ambapo tarehe hiyo mwaka
huu alikuwa anatimiza miaka 63.
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
-Amen
No comments:
Post a Comment