Huduma za benki nchini Somalia
Serikali ya Somalia imesema kuwa uamuzi wa benki moja nchini
Marekani kufunga akaunti za kampuni za kuhamisha fedha nchini Somalia utaathiri
usalama ulioafikiwa nchini humo.
Benki ya Merchants kutoka jimbo la Carlifornia,ambayo
husimamia asilimia 80 ya fedha zote zinazoelekea nchini Somalia, imesema kuwa
inaondoa huduma zake nchini humo kutokana na madai ya mapya ya biashara ya
fedha chafu.
Mwakilishi wa umoja wa mataifa nchini Somalia Nicholas Kay
,amesema kuwa hatua hiyo inaleta wasiwasi mkubwa kwa kuwa usafirishaji huo wa
fedha ndio mfumo wa maisha ya raia wa Somalia.
Raia wa Somalia nchini Marekani hutuma nyumbani zaidi ya
dola millioni 200 kila mwaka.
No comments:
Post a Comment