Pages

Monday, February 16, 2015

Boko Haram waondoka Gombe

Wapiganaji Waislamu wa Boko Haram wametoka katika mji wa Gombe kaskazini-mashariki mwa Nigeria baada ya mapambano makali na jeshi.
Wakuu wanasema wapiganaji wamerejeshwa nyuma, lakini ripoti nyengine zinasema kuwa wapiganaji hao waliondoka kwa hiari yao.
Boko Haram waliingia Jumamosi asubuhi katika 


vitongoje vya Gombe baada ya kushambulia mji jirani wa Dadin Kowa.
Wapiganaji hao wamewahi kufanya mashambulio ya kujitolea mhanga katika mji wa Gombe, lakini hawakupata kujaribu kuuteka mji wenyewe.

Nigeria ikitarajiwa kufanya uchaguzi tarehe 14 Februari, lakini umeakhirishwa kwa majuma sita kwa sababu ya wasiwasi kuhusu usalama.

No comments:

Post a Comment