Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, February 12, 2015

FANYA HAYA KAMA KAMA UMEPATA KAZI SEHEMU MBILI TOFAUTI

Unajisikiaje kupata kazi sehemu mbili tofauti? Inaonyesha juhudi zako za kutafuta kazi zimezaa matunda. Lakini unahitajika kuamua ni kazi ipi uchukue, ingawa watu wengi tunapenda kuangalia hela kwanza kabla ya vitu vingine.

Hivyo kazi yenye mshahara mkubwa ndio utakayoichagua. Je mshahara mkubwa unakupa tumaini gani? Kuna mambo mengine ya kuzingatia pia, kama kuna maslahi mengine ya kiafya, elimu na familia yako kwa ujumla.
Unapochagua kazi inakubidi uangalie faida na hasara ya kila kazi utakayoiendea kwa kuangalia mahitaji yako ya muda mfupi na mahitaji yako ya muda mrefu.


Thibitisha kabla ya kuchunguza

Hi inamaanisha kwamba jitahidi kujua kampuni hii ina nini ndani yake? ili usifanye makosa, utafanya kazi wapi na mshahara ni shilingi ngapi?




Zingatia mshahara kwa ujumla wake

Mshahara ni sehemu ya fedha ambayo inahusisha mshahara wenyewe, marupurupu, mgawanyo wa faida na vitu vingine. Kuna vitu vingine ambavyo si fedha kamili ila vina thamani kama, matibabu, daktari wa meno, pensheni, hivyo vyote vinaongeza uthamani wa kazi unayotakiwa kuichukua na kama utataka kuvitumia.


Zingatia vitu vingine ambavyo si fedha kabisa
Je kufanya kazi ukiwa nyumbani angalau siku moja kwa wiki ni muhimu kwako? Au heshima unayopewa kwenye kazi hiyo kama cheo huwezi kusema ni fedha kiasi gani ila ni sehemu ya mambo ya kuzingatia. Je muda wako wa kazi umekaaje? Unatakiwa kufanya kazi miezi mingapi kwa mwaka? Je unapandaje cheo na kupata nyongeza? Je utakuwa unatoa ripoti zako kwa nani na kwa muda gani? Je ni watu wangapi wanaripoti kwako?

Vile vile angalia hivyo vitu ambavyo si sehemu ya ofa uliyopewa;

Inakubidi uangalie kwa umakini vitu ambavyo huwa havitajwi kwenye mkataba, mfano wafanyakazi na mabosi wako utakaowakuta. Kama unapenda kupata bosi mpya au hapana, lazima siku moja upande cheo au uelekee ngazi nyingine. Je utamaduni wa hilo shirika unaendana na hulka na tabia zako? Je unawezaje kufanya kazi kwenye kampuni kubwa au dogo?

Kuna baadhi ya vitu vya kuzingatia kama mavazi, na mwonekano wa kila siku hayo ni mambo yanayoonekana. Hayo mambo mara nyingi hayaandikwi kwenye matangazo ya kazi. Lakini yana nguvu sana katika utendaji na maisha yako ya hapo kazini, hivyo fanya uchunguzi wa kina kabla ya kufanya maamuzi ya kukubali kazi au kuikataa.

Tofautisha mahitaji ya msingi na yale yasiyokuwa ya msingi. Labda ngoja nikupe maana ya mahitaji ya msingi ni vile vitu ambavyo lazima uwe navyo na yale yasiyokuwa ya msingi ni vile vitu ambavyo ni vizuri kuwa navyo ila si lazima. Ukiwa na uelewa huo utakusaidia kufanya maamuzi ipasavyo na kwa usahihi.
Je ni kiasi gani cha chini kabisa ambacho unaweza kulipwa? Hata kama utapata kazi ishirini ila hazikusaidii kwenye kiwango cha chini cha uhitaji wako ni kazi bure. Kiwango chako cha chini itategemea na mahitaji yako Kama umekuwa huna kazi kwa muda mrefu hela kwako ni tatizo. Hivyo uwe tayari kupata mshahara wa kawaida kuliko mategemeo yako makubwa, ingawa ni mpaka pale utakapoweza kujua kiwango chako cha chini unachoweza kukubali ili kujua uchukue kazi au usichukue kazi hiyo na labda uendelee kutafuta kazi nyingine.

Malengo ya Muda mfupi na Malengo ya muda mrefu
Wakati mwingine kazi mpya itaathiri maisha yako ya baadaye. Ingawa watakufanyia mafunzo maalumu na kuongeza ujuzi ili uweze kuendana nao, hivyo unatakiwa kuamua kwamba kama ni kitu unachokihitaji maisha yako yote au ni cha muda mfupi.

No comments:

Post a Comment