Pages

Monday, February 9, 2015

HAYA NDIO MAMBO YA KUFANYA KAMA UNATAKA FOLLOWERS WENGI INSTAGRAM



Labda kama wewe ni staa, lakini kama ni mtu wa kawaida, kupata followers wengi kwenye Instagram sio rahisi. Lakini haya ni mambo kadhaa ambayo ukifanya huenda followers wakaongezeka.


1. Caption
Beyoncé huweka picha nzuri sana kwenye Instagram lakini kama angekuwa anaziwekea caption, zingependeza zaidi. Hata hivyo huyo ni staa tayari hivyo hili linaweza lisiwe na madhara sana kwake. Caption huzipa uhai picha zako na kama utaziandika kwa ubunifu, ni rahisi kupata likes na hata follows nyingi.

2. Hashtags

Hashtags zina kazi zake maalum. Hashtags ni njia nzuri za kuvuta traffic kwenye picha zako lakini zifanye zihusiane na picha – kwakuwa zikiwa nyingi zinaweza kuwakera followers wako.

3. Selfies

Selfies ni nzuri kupost hapa na pale. Ukiziweka nyingi na tena ambazo hazina mvuto unaweza kuishia kuchezea unfollow za kutosha kwa kuijaza tu timeline.





4. Weka picha zenye ubora
Siku zote weka picha nzuri zaidi. Chagua picha kali.

5. Zikusanye

Badala ya kumwaga picha kumi zenye muonekano unaofanana au eneo moja, ziunganishe na upost kama picha moja.

6. Repost

Kuna picha nzuri unayoweza kuiona kwenye akaunti ya mtu mwingine. Irepost ili watu wanaokufollow waweze kuiona pia.

7. Like!

Usiwe mtu wa kupost tu picha na kuondoka. Chukua muda wa kulike pia picha za wengine au kucomment pale unapoguswa.

8. Screenshots Whatsapp

Unaweza ukawa umechat na mtu kwenye whatsapp na mazungumzo hayo kuwa na kitu cha kufurahisha. Unaweza ukaipost ilimradi tu isiwe na ujumbe wenye utata.

9. Chakula, wanyama, watoto

Tunaona watu wengi wakipost picha wakiwa mezani wakila chakula kitamu, kupost picha za wanyama wanaowafuga au za familia zao. Kikubwa ni kuweka kwa kiwango.

No comments:

Post a Comment