Nimefikia uamuzi wa kudai talaka kutokana na kuchoshwa na
vitendo vya ukatili nilivyokuwa nafanyiwa na mume wangu, kwa zaidi ya miaka8 na
hata sasa bado anaendeleaje, Kwani hata kuongea uongo kwenye media juu yangu ni
ukatili pia.. nimekuwa nikinyanyaswa kijinsia na
mume wangu na sikuwahi kutoa taarifa mahala popote kutokana
na vitisho alivyokuwa akinitisha.
Watu Wengi wanafikiri nilikuwa na ndoa nzuri sana
lakini
kumbe nilikuwa Nikivumilia tu Kwani niliamini ipo siku atabadilika maana
nilimpenda sana mume wangu.Nilijaribu kuficha huzuni na maumivu yangu kila
nilipotoka na mume wangu kwenda kwenye Huduma au mahala pengine penye
mkusanyiko wa watu.
Sijawahi hata Mara moja kutoa taarifa hata kwa wazazi wangu
juu ukatili niliokuwa nafanyiwa na mume wangu.Kwanza sikutaka kumvunjia heshima
kwa ndugu zangu na pia alikuwa akinitishia kuniua na kuongeza kunifanyia ukatili
huo.
Kutokana na historia yake ya nyuma alikuwa na uwezo wa
kunifanya chochote na ndiyo maana nilikuwa nikimwogopa sana.
Siku zote nilikuwa akilala na panga kitandani ambalo ndilo
alikuwa akinipiga nalo na kuapa kunichana chana Mwili Kabla ya kuniua.
Kipigo hicho nimekuwa nikikipata hata ninapokuwa kwenye
Huduma bila kujali natakiwa kuwa kwenye mood nzuri ili ni perfome vizuri.
Nimevumilia muda mrefu lakini ndo mateso yakawa yanazidi na
kufikia hatua ya kufukuzwa akidai yeye ana mwanamke mwingine wa dini yake ya
zamani hivyo anataka amlete hapo nyumbani.
Nilikataa kuondoka na kumwambia amlete tu, tutaishi wote
mimi nitakuwa nikilala chini maana nshazoea siku zote Amekuwa akinilaza chini
,alivyoona siku zinazidi kwenda na mimi nimegoma kuondoka basi akaamua sasa
isiwe siri ya chumbani tena Akawa ananitoa ananipigia sebuleni na anasema
nataka mtoto na wengine wote wajue kuwa huwa nakupiga humu ndani.Ikafika hatua
anataka kunitoa nje ya geti ili majirani wajue kuwa huwa napigwa na anifukuze
mbele yao.
Kwa Miaka yote alinizuia kufungua account bank na kudai kuwa
yeye ndo mwanaume hivyo pesa zote ataweka yeye. So pesa zangu zote nilizokuwa
naingiza alikuwa akichukuwa yeye na kuzihifadhi kwa account yake binafsi.
Sikuwa nikibaki hata na mia.Nilijaribu kufanya biashara
lakini napo pesa zote akawa akichukuwa yeye ikabidi niache.. Nikitaka hata
vocha ya mia tano Lazima nimwombe hela na niitolee maelezo ninampigia nani.
Mume wangu kwa kipindi chote hakuwahi kuwa na kazi yoyote
zaidi ya kunifanya mimi ndo biashara yake. Lengo lake ilikuwa ni kunitumia mimi
kwa maslahi yake na sio upendo kama mke wake.
Hakuwahi kunipenda hata yeye mwenyewe hukiri kuwa alinioa tu
basi ili afanikiwe kwenda ulaya kwa kuwa mimi nilikuwa nikisafiri na babu
yangu.
Na yeye kila akijaribu kwenda nje anashindwa. Kuna mambo
mengi ya ukatili aliyokuwa akiyafanya ndani siwezi kuyasema kwa ajili ya
maadili na pia bado Ninamheshimu kama mzazi mwenzangu. Alipoona siondoki pamoja
na vipigo, matusi na kunifukuza kote.
Akasema nitahakikisha nakufanyia jambo ambalo utaondoka
mwenyewe humu ndani bila kupenda sitaki kuzungumzia suala ambalo liko mahakani
ingawa hilo nahisindilo alilokuwa kadhamiria ili tu niondoke.
Nilijaribu sana kumsihi tukae kikao na wazee ili watushauri
na kutusaidia lakini nilikuwa nikiambulia matusi tu ya nguoni ambayo siwezi
kuyaandika hapa.
Siku niliyoondoka nyumbani alidhamiria kuniua alidai hata
akiniuà hakuna atakaye amini kuwa ni yeye kaniua, na ni kweli maana sikuwahi
kushtaki mahala popote.
Alichukuwa panga akanipiga nalo kisha akaniniga hadi
nikaishiwa nguvu .Aliponiachia sielewi nilitokaje ndani. Ugomvi mkubwa
ulitokana na mimi kukataa kufanya tenda la ndoa kinyume na maumbile.
Amekuwa Alinipiga na kunilazimisha kufanya tenda hilo
kinyume na maumbike kwa miaka mingi lakini nikisema bora nife kuliko kutendewa
ukatili huo.Amekuwa akidai kuwa wanawake tumeumbwa ili tufanyiwe tenda hilo la
ndoa mbele na nyuma so ni haki yake.
Niliondoka kwake nikiwa na sh elfu mbili tu. Nilimwachia
kila kitu nyumba gari na pesa zote zikiwa kwa account yake zaidi ya milioni
50.Sikuwa na uwezo wa kutoa pesa maana ni account yake binafsi.
Nimejitahidi sana kumwita kwenye vikao hata vya familia ili
tu tujaribu kuzungum za lakini amekuwa akionesha dharau tu na kusema yeye
haitaji ndoa tena anaoa mke mwingine hivyo hawezi kusuluhishwa.
Ingawa Amekuwa akidanganya sana kwenye media. Nilimwuliza
Unapata faida gani unapodanganya watu kuhusu mimi?
Akasema yeye amechafuka kwa ubakaji so acha na mimi
nichafuke na akasema atahakikisha sifanyi huduma sehemu yoyote labda nihame
nchi.
Kama msg hizo angekuwa amezituma bila kuandika na matusi
ningezikopi but zaidi kauli zake ni za matusi. Hivyo imefika mahali nimeona
bora tuachane kisheria na pia nipate haki yangu maana mume wangu anajivunia
mali ambazo hakuzitolea jasho yeye na huku anawatapeli watu kwa kudai kuwa hana
pesa maana mimi nimeondoka nazo wakati ni uongo mtupu.
Mimi ninapanda daladala siku hizi sababu sina uwezo wa kuwa
na gari hadi niazime kwa marafiki zangu. Mume wangu amekataa hata kumsomesha
mtoto sasa hivi nahangaika kutafuta ada ili mtoto arudi shule lakini pesa
yote anayo Mbasha.
Sasa sijui hapo ananikomesha mimi au mwanaye.!maana urithi
wa mtoto ni elimu bora na mzazi anayempenda mwanaye atapambana ili kuhakikisha
mtoto anapata elimu bora.
Nilikaa kimya muda mrefu sikutaka kuzungumza lakini imefika
mahali Nimechoka maana huyu bwana hajiheshimu. Tukikutana anasema sio yeye
anayepeleka habari mitandaoni.
Ninaomba wanaume wenyewe Mfano wake waache kuwafanyia
ukatili wake zao majumbani.Najua wako Wengi sana wanao nyanyasika kama ilivyo
kuwa kwangu lakini Hawana sehemu za kukimbilia Hivyo wanavumilia tu na mwisho
wa siku wanakufa na kuacha watoto wakiteseka.
Mimi Nilivumilia zaidi ya Miaka 8 lakini imefika mahali
enough is enough. Maandiko matakatifu yanasema, ndoa haivunjwi isipokuwa kwa
uasherati.
Acha nife kwa mapenzi ya Mungu na sio kwa mapenzi ya mtu..Na
ni naamini sitakufa mpaka ndoto zangu zitimie.
Mume wangu ameapa kuwa atahakikisha sifanyi Huduma tena
lakini ninasema katika Jina la YESU, kama Bwana aishivyo, mwanzilishi wa huduma
yangu ni Mungu Hivyo mmalizaji wa Huduma yangu ni Mungu mwenyewe.
Na sasa ninajipanga kumwimbia Mungu kama sitaimba
tena.Wakati mwingine usipokuwa mwangalifu ndoa inaweza kukukosesha ufalme wa
mbinguni hasa Ukiingia kwenye ndoa isiyo sahihi. Ninampenda sana mume wangu
lakini ninampenda Mungu wangu zaidi. Ahsante.
Nimeamua kuandika Maana Nimechoka kuficha maovu aliyokuwa
akinitendea.Nimemtunzia heshima muda wote maana sikutaka jamii imjue ni mtu wa
aina gani but yeye anatumia ukimya wangu kama udhaifu so naona bora niweze wazi
ili jamii imtambue mimi yamenikuta najua Wapo Wengi tu wanapitia mateso
niliyoyapitia mimi.
Kutokana na vitisho wanaendelea kunyanyaswa. That is not
fair kwa kweli.Mimi ningekufa Kabla ya wakati wangu lakini namshukuru Mungu
niko hao hata sasa na pia ili kuwaonya wanaume wanaume wenyewe tabia kama yake.
Kama umemshoka mwanamke achaneni kwa amani sio kumnyanyasa
mwanamke kama alivyokuwa anafanya Mbasha kwangu.
Ninapinga vikali unyanyasaji wa wanawake na watoto
majumbani.
No comments:
Post a Comment