Moja kati ya vyakula vinavyomletea mlaji wake harufu kali ni
vitunguu swaumu ambavyo huumika kama viungo kwenye chakula .
Vitunguu swaumu vina vitu Fulani ndani yake amvayo
hujitokeza pale kinapokatwa , kusagwa au hata kutafunwa vitu hivi kitaalamu hufahamika kama Allicin
na Allin na hivi ndio hasa husababisha harufu kali ambayo hutokea baada ya mtu
kula vitunguu swaumu au vyakula vilivyoungwa kutumia vitunguu swaumu .
Vitunguu swaumu pamoja na faida zake ka afya ya binadamu
husababisha harufu mbaya mwilini.
Pamoja na hayo vitunguu swaumu vina faida kubwa sana mwili
mwa mwanadamu na faida hizo huletwa na hii Illin ambayo inatajwa kuwa sababu ya
harufu yake mbaya na moja kati ya faida zake ni jinsi ambavyo vitunguu swaumu
husaidia kupambana na bacteria wanaoleta magonnjwa mbalimbali na virusi tofauti
.
Mbegu ya Binzari
Mbegu ya Binzari
hutumika kwenye mapishi ambapo
huleta ladha nzuri kwenye chakula , hata
hivo mbegu hizi husababisha harufu mbaya ambayo inabakia mdomoni kwa muda mrefu
. Kama unataka kupunguza harufu mbaya unaweza kuipunguza kwa kunywa maji mengi
na kutumia vyakula vingine ambavyo vinatumika kupunguza harufu ambavyo havina
harufu kali .
Nyama Nyekundu .
Nyama nyekundu ni moja kati ya vcyakula vinavyosababisha
harufu mbaya mdomoni na tumboni . Ni vigumu kwa wtau wengi kukubaliana na hili
kwa kua nyama nyekundu ni moja kati ya vyakula vinavyopendwa sana na watu .
Tafiti zinaonyesha kuwa jasho jingi ambalo husababishwa na mafuta yanayoganda
mwilini kutokana na ulaji wa nyama nyekundu ni moja kati ya vitu ambavyo huleta
harufu mbaya kwenye mwili wa mwanadamu .
Nyama nyekundu ni moja kati ya vyakula sugu kwa kusababisha
harufu mbaya mdomoni na inayotokea tumboni .
Kama unataka kupunguza harufu kutokana na nyama nyekundu ni
vyema ukapunguza na kuanza kula nyama itokanayo na samaki na wanyama wengine wa
baharini .
Mboga Za Majani
Baadhi ya mboga za majani zinasababisha harufu mbaya mwilini
nazo ni cauliflower , kabichi, broccoli na nyinginezo nyingi .
Tunashauriwa kula mboga za majani kwa wingi kwa sababu
hazina mafuta na zinaongeza vitamin mwilini lakini zina madini aina ya sulphur
ndani yake ambayo husababisha harufu mbaya .
Kahawa
Kahawa nayo iko kwenye orodha ya vyakula ambavyo
vinasababisha harufu mbaya mdomoni na mwilini kwa jumla . Moja vitu ambavyo
vimo ndani ya kahawa ambavyo ni Caffeine husisimua mfumo wa neva yaani ile
mishipa ya fahamu mwilini na husababisha mtu avuje jasho kwa wingi kuliko
kawaida .
Pia ile acid ambayo iko ndani ya kahawa hufanya mate yakauke
mdomoni na hapo bacteria na vijidudu vingine vyenye kufanya harufu mbaya iwepo
mdomoni hujitokeza kwa wingi . Kutafuta Big G huweza kusaidia kutatua tatizo
hili , tafuna Bgi G mara tu baada ya kunywa kahawa na hapo utazuia harufu mbaya
mdomoni.
No comments:
Post a Comment