Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma |
Chanzo cha kuuawa huyu askari ni kwamba alipigiwa simu na Mtendaji wa Mtaa wa chang’ombe juu hapa Dodoma Mjini akimjulisha kuwa amepokea taarifa ofisini kwake kutoka kwa OLIVER BALTAZARI, MIAKA 52, MKAZI WA CHANG’OMBE JUU kuwa kijana wake aitwaye TISI S/O SIRILI MALYA ana mtesa motto wake mdogo wa miezi nane aitwaye VALERIAN TISI MALYA na anahisi labda ameshamuua kwani motto huyo halii tena.
Alichofanya mtendaji huyu ni kumpigia askari wetu huyo simu naye akaenda hadi katika Ofisi ya huyo Mtendaji wa Mtaa. Waliongozana wote wakiwa pamoja na kijana mmoja hadi anakoishi huyo TISI SIRILI MALYA. Walipofika askari aligonga mlango akijitambulisha kuwa yeye ni askari hivyo atoke nje.
Alichofanya mtuhumiwa huyo ni kumnyanyua mtoto wake mdogo wa miezi nane kwa mkono mmoja miguu juu kichwa chini na kutaka kumkata kwa panga na kusema namkata shingo na sitaki kuona mtu.
Askari aliamua kumwokoa mtoto huyo na alipomrukia mtuhumiwa kwa bahati mbaya aliteleza na ndipo mtuhumiwa akamkata kichwani askari wetu na akadondoka chini kutokana na jeraha kubwa alilomsababishia. Hata hivyo mtuhumiwa huyo aliendelea kumkatakata na Mtendaji na kijana waliyekuwa naye ambaye ni maratibu wa watoto wanaoishi katika mazingira magumu iliwabidi kukimbia huku wakipiga kelele kuomba msaada.
Mtuhumiwa baada ya kufanya kitendo hicho cha kinyama alikimbia huku nguo zake zikiwa zimetapakaa damu akiwa na panga mkononi.
Askari huyu muda mfupi kabla ya tukio hili alikuwa ametokea katika kituo cha Redio cha Dodoma FM kwa ajili ya kuandaa kipindi cha kuielimisha jamii juu ya ulinzi wa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) tunapoelekea kipindi cha uchaguzi, kwani mbali na kazi anazofanya mojawapo ni kushiriki katika vipindi vya kutoa elimu ya Polisi Jamii hapa mkoani Dodoma.
Msako bado unaendelea ili kuweza kumtia nguvuni mtuhumiwa huyu aliyesababisha kifo cha askari wetu wakati alipojitolea maisha ya ili kumwokoa huyo mtoto mdogo.
Tuinazidi kuomba msaada wa wananchi popote pale watakapomuona TISI S/O SIRILI MALYA, MIAKA 29, MCHAGA ambaye ni maji ya kunde, mwembamba, siyo mrefu sana saizi ya kati alikuwa amevaa suruali rangi ya blue iliyopauka na T-Shirt rangi ya dark blue na kofia nyeupe yenye alama nyekundu ili tuweze kumkamata na kumfikisha mahakamani.
Imetolewa na:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi - Misime D.A (SACP)
No comments:
Post a Comment