Pages

Friday, February 6, 2015

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE KASI KULIKO WOTE NDANI MANCHESTER UNITED

 Katika hali ya kawaida kasi ni sehemu kubwa ya mchezo wa soka katika zama hizi na moja kati ya sifa ambazo humpambanua mchezaji bora na yule asiye bora ni jinsi ambavyo wachezaji wanatumia kasi wakiwa uwanjani kwa faida ya timu zao.
Beki wa Manchester United Chris Smalling ni moja kati ya wachezaji ambao wamekuwa wakilaumiwa na mashabiki wa timu hiyo kutokana na ubovu wa safu ya ulinzi ya United ambayo imekuwa ikiruhusu sana mabao kufungwa .
Ni vigumu kuamini kuwa beki huyu ambaye alijiunga na United miaka minne iliyopita leo hii ndiyo mchezaji mwenye kasi kuliko wote kwa mujibu wa takwimu za klabu hiyo .
Chris Smalling ndio mchezaji mwneye kasi kuliko wote ndani ya Man United.
Hii ni siri iliyofichuliwa na mshambuliaji wa Manchester United James Wilson ambaye salisema kuwa kuna wachezaji wengi wenye kasi kwenye timu hiyo lakini hakuna anayemzidi Chris Smalling.

Wilson amezungumza haya kwenye mahojiano maalum ambapo alisema kuwa wanapokuwa uwanjani huwa wanavalishwa vifaa maalum vya GPS ambavyo kwa msaada wa teknolojia ya kisasa humsaidia kocha na wasaidizi wake kutambua jinsi wachezaji wanavyofanya mazoezi pamoja na kasi waliyo nayo na umbali ambao wanakimbia .
Kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa na kifaa hicho hakuna mwenye kasi kama Chris Smalling ndani ya kikosi cha Man United .

James Wilson pia amewataja wachezaji wengine kama Ashley Young , Luke Shaw Antonio Valencia pamoja na yeye mwenyewe kama wachezaji wengine wenye kasi lakini bado hakuna anayemzidi Smalling.

No comments:

Post a Comment