Japan imeyataja mauaji hao kuwa kitendo cha kikatili ambapo
waziri mkuu wa Japan mwenye hasira amesema kuwa japan itaendela kushirikiana na
nchi zinazopambana na kundi hilo.
Wiki moja iliyopita mateka mwingine raia wa Japan Haruna
Yukawa aliuawa na wanamgambo hao.
Familia ya Kenji Goto
Kanda ya video ya hivi punde inafanana na zile zilizokuwa
zikionyesha kuuawa kwa mateka wengine awali.
Kenji Goto ambaye ni mwandishi wa habari alitekwa nyara
nchini Syria mwezi Oktoba mwaka uliopita.
No comments:
Post a Comment