Mchungaji Mchungaji Josephat Gwajima
|
Nakala ya barua kutoka kwa Meneja wa Mkoa wa Kinondoni wa
NHC.
KANISA la Mchungaji Josephat Gwajima lililokuwa likiendesha shughuli katika
viwanja vya Tanganyika Packers Kawe,
wilaya ya Kinondoni, jijinI Dar limeamriwa kuondoka eneo hilo.
Kanisa hilo ambalo kwa muda mrefu limekuwa likiendesha shughuli zake eneo hilo
limedaiwa kusababisha usumbufu na kero kubwa za makelele kwa wakazi wa maeneo
hayo.
Barua iliyosainiwa na Meneja wa Mkoa wa Kinondoni wa Shirika
la Nyumba la Taifa, B.N. Masika, imesisitiza kwamba pamoja na
kutambuliwa umuhimu wa kanisa hilo kuendesha
shughuli zake shirika hilo
halitaweza kutoa ruhusa kwa kanisa hilo kuendelea kufanya mahubiri katika viwanja hivyo,kwani shirika
hilo limeshaanza kutumia viwanja hivyo
kwa maendeleo ya wananchi wa Kawe ikiwa ni ujenzi wa makazi n.k
Barua hiyo imetoa 30
zinazoishia tarehe 9 Machi mwaka huu
ili Mchungaji Gwajima ajitayarishe kuondoka eneo hilo.
No comments:
Post a Comment