Mwanamume aliyejitolea kuuza ubikira wake wakati wa
maadhimisho ya siku ya wanawake duniani
Mwanamume mmoja amejitolea kutoa ubikira wake wakati wa
maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake.
Sorin Gorgian Salinievcici mwenye umri wa miaka 24
amejitolea kuuza ubikira wake kwa pauni 1,476 baada ya kusoma kuhusu wanawake
wanaofanya hivyo.
Alielezea kuwa :''mimi husoma kuhusu wasichana wanaofanya
hivyo na nikafikiri kwamba iwapo wanafanya hivyo hata mimi naweza kufanya''.
Amesema kuwa mwanamke yeyote atakayenunua ubikira wake ni
sharti awe mwenye heshima.
''Sisemi kuwa ni lazima awe mrembo lakini awe mwanamke wa
kawaida, mzuri na mwaminifu''.alisema.
Katika bango aliloandika nyumbani kwake huko Romania,alisema
kuwa inaweza kuwa zawadi nzuri katika maadhimisho ya siku hiyo ya wanawake
mnamo mwezi machi tarehe 8.
Je,unadhani kitendo hiki kinakubalika?
No comments:
Post a Comment