Pages

Monday, February 16, 2015

Maneno Ya TID kwa Q Chief : “Kaanzisha bendi yake ikwapi? hana hata gitaa vitu vyote kauza… am not stupid yeye ndio stupid,”

Baada ya siku ya jana kujibiwa na Q Chief juu ya coment aliyoitoa baada ya kuulizwa swali juu ya kilichopelekea kuvunjika kwa Top Band TID nae atoa yake ya moyoni,

Q Chief aliongea mengi sana moja wapo ilikuwa ni kuhusu kutokusikia kwa Top Band ikifanya chochote kwa sasa na kumsihi TID aache unga, aangalie wazazi wake na familia yake kwa ujumla huku akidai kuwa yeye kashaacha unga, Tid amemjibu kwa kusema

“mimi ndio hela zangu, album yangu, yaani kitu changu yeye kaja kuomba kufanya kazi tu, namlipa kama mshahara wake tu sio kwamba yeye ni part of it hapana.hicho ndio alichokosea yeye, hio ndio tatizo lake,
yaani … mi nataka watu wajue hivyo. ebwana yule kaja bana mi kuimba kuimba kwenye bendi yangu, sawa sawa, nimekuingiza kwenye album kwenye wimbo mmoja, tumefanya wimbo, nimeenda kwa muhindi mimi, nimechukua hela mimi, nimekukabidhi hela kama malipo yako, baadae eti unakuja kuniambia eti ebwana katika zile milioni kumi mimi bwana huwezi kunipa milioni kumi bwana sio kitu chako wala nini, yaani wewe ur just a featuring.hicho ndio kitu mi ninachomshangaa anachanganyikiwa.”


mimi halafu nilivyokuwa mstaaru amenichukulia na polisi nini, anataka milioni nne, nikachukua hela nikampa kaanzisha bendi yake ikwapi? ana bendi sasa hivi? hana hata gita vitu vyote kauza, mimi ukija kwangu sasa hivi kuna kila kitu, hadi waya wa kuchomeka sijauzaaaa, hadi vile vya mwanzo na nilivyonunua tena vipya juzi  uingereza sijauza am not stupid yeye ndio stupid. halafu yaani daah ebwana jamaa amenipakazia kweli rafiki yangu, hadi mama angu ametaka kulia, nimeenda nyumbani mi nilikuwa sijui heee umerudi mama sasa hivi, halafu mimi sasa nilikuwa nakazi natakiwa niende studio ku-record, yaani jamaa anazidi kunichengua ananitoa kwenye mood, mama akaniambia “ndio nini sasa,” was like mom, nilikuwa nafanya interview tu Casto kaniuliza swali.

No comments:

Post a Comment