Pages

Monday, February 16, 2015

Mapya yenye utata yaibuka waliofariki kwa ajali ya moto


Wakati zikiwa zimepita siku sita tangu yafanyike mazishi ya ndugu sita wa familia iliyoteketea kwa moto eneo la Kipunguni A jijini Dar es salaam , mapya yameibuka na kuzua utata kwa ndugu na jamaa wa familia hiyo.
Watu hao ambao ni ndugu wa Waziri Ofisi ya Rais, Kazi Maalum, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Maluum, Profesa Mark Mwandosya, walizikwa Februari 10, mwaka huu katika makaburi ya Airwing Ukonga, kufuatia nyumba yao kuteketea kwa moto wakati wakiwa wamelala.



Mazishi yao yaliyohudhuriwa na mamia ya wananchi, Makamu wa Rais Mohamed Gharib Bilal, baadhi ya mawaziri na wabunge.
Katika tukio hilo, dada wa Profesa Mwandosya, Celina Yegela (50), mume wake Kapteni mstaafu wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) David Mpilla (65) na mdogo wake Samuel Yegela (30), waliteketea kwa moto
Wengine ni mtoto wao Lucas Mpira (36) wajukuu  wao Celina Emmanuel (9) na Paulina Emmanuel (5).
Hata hivyo, mtoto mmoja wa familia hiyo Emmnuel Mpilla alinusirika baada ya kuwa nje wakati tukio hilo linatokea.
MAPYAI YAIBUKA
Wakati ndugu wa familia ya Yegela na Mpilla wakitafakari juu ya msiba huo mzito, imeibuka taarifa ya kuwapo kwa mwanamke  (jina linahifadhiwa) anayedai kuzaa watoto wawili na marehemu Mpilla.
Habari za uhakika kutoka ndani ya familia hiyo, zinasema uwapo wa watoto hao umezusha mtafaruku kwa pande hizo za familia hiyo.
Upande wa familia ya Yegela anakotoka Profesa Mwandosya ukisisitiza kutowatambua huku familia ya Mpilla ikoonyesha kuwatambua.
Watoto hao walijulikana kwa majina ya Kabuta Mpilla  anayesoma Shule ya Sekondari ya Juhudi iliyopo Ukonga na Neema Mpilla ambaye bado hajaanza masomo.
Aidha, taarifa kutoka kwa marafiki wa karibu na wanafamilia wa Mpilla zinaeleza watoto hao walianza kutambulishwa kwa siri na baba yao kabla ya kifo chake.
“Suala hili liliibuka wakati tunakwenda kwenye mazishi ya marehemu wetu,  hatukutaka kufuatilia kwa undani kwa sababu tuliamini kama wapo basi watajitokeza tu,” alisema mmoja wa wanandugu hao.
Hata hivyo ndugu huyo alisema baada ya mazishi ya wapendwa wao,walilifikisha suala hilo katika vikao vya kifamilia, lakini upande wa Yegela walikataa kutoa sababu za msingi kwamba wakati wa uhai wa dada yao hawakumsikia akizungumzia jambo la aina hiyo.
Msimamo huo umeonekana kuigawa pande hizo, huku familia ya Mpilla ikionekana dhahiri kukubali wakisema watoto hao watamuondolea unyonge Emmanuel ambaye kwa sasa hana wazazi wala ndugu waliobaki.
 “Kitu kizuri mama wa watoto hawa hakusema anataka kuingizwa kwenye mirathi, tunachoona hapa watoto hawa watamtoa ukiwa kaka yao, haya ni maoni yetu tu lakini hatuwezi kusema chochote kwa sasa,” alisema mwanafamilia mmoja wa Mpilla.
Baadhi ya rafiki wa karibu wa marehemu Mpilla waliozungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa majina yao, walikiri kuambiwa jambo hilo na marehemu kuwa ana watoto wengine nje ya ndoa.
Walisema kati ya watoto hao, Kabuta ambaye alipewa jina hilo baada ya mtoto wao wa kwanza aliyeitwa jina hilo aliyezaa na marehemu Celina kufariki kwa kugongwa na gari.
Hata hivyo wasemaji wa pande hizo mbili hazikuweza kupatikana kuzungumzia suala hilo.
Gazeti hili ilifanikiwa kumpata mwanamke anayetajwa kuzaa watoto hao kupitia simu yake ya mkononi, ambapo  alipoulizwa ukweli wa suala hilo alikanusha kwa kusema hana watoto kama hao.
“Wewe amekuambia nani suala hili?......jamani mimi watoto wangu sijazaa na marehemu Mpilla unayemsema, nakuomba sana sitaki usumbufu,” alisema na kukata simu

No comments:

Post a Comment