Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, February 16, 2015

MBOWE:TUTAHAKIKISHA KILA MWANANCHI AMEJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA MPIGA KURA

Mwenyekiti wa Chadema Freman Mbowe akiwa anasoma hotuba wakati wa ufunguzi wa mkutano wa viongozi wa  chama hicho wa kanda ya kaskazini uliofanyika katika  hotel ya new Arusha jijini hapa.

viongizo wa chadema  akiwemo mwenyekiti wakiwa wanasali kwanza kabla ya mkutano wa viongozi wakanda ya kaskazini kuanza


 Naibu katibu mkuu wa Chadema Salum Mwalimu akiwa anaongea nawaandishi wahabari.

 MWENYEKITI wa chama cha demokrasi na maendeleo Chadema Freeman Mbowe amesema kuwa  chama chao kimejipanga kuahakikisha kinahamasisha  kwa  nguvu zote wananchi weweze kwenda kujiandikisha katika  daftari la mpiga
kura. 

Alisemakuwa hii itaweza kumsaidia kila mwananchi  kuweza kupata haki yakumchagua
kiongozi bora  anaemtaka  katika uchaguzi mkuu ujao  wa kuwachagua viongozi wakuu ambao ni rais, wabunge na madiwani.


Alisema kuwa pamoja ya kuwa tume wamekuwa wananchelewesha kufanyika kwa zoezi hili, wao wamejipanga kikamilifu na pindi ambapo zoezi hili litatangazwa  kuanza rasmi watajitaidi kwa njia yoyote kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha.

Alisema kuwa kwa upande wa kupiga kura katiba wanaendelea na msimamo wao ambao walitangaza awali wa kutoshiriki katika mchakato wa kura ya maoni ya katiba  huku akisisitiza kuwa swala la kutoshiriki katika mchakato wakura za maoni auingiliani kabisa na kuhamasisha wananchi kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura. 

Alimaliizia kwa kuwasihi wananchi wajitokeze kwa wingi  sana pindi pale ambapo watasikia zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la kudumu limewadia  ili waweze kupata haki yao ambayo itawaruhusu kuchgua kiongozi wanao wataka.

Habari kwa hisani ya libeneke la kaskazini blog

No comments:

Post a Comment