Afisa wa kampuni ya kutengeza mipira ya kondomu katika
ufalme wa Thai akagua mipira hiyo
Maafisa wa afya katika ufalme wa Thai wamesema kuwa wavulana
ambao wanaogopa kuchagua mipira ya kondomu zinazowatosha vizuri ndio chanzo cha
mlipuko wa magonjwa ya zinaa miongoni mwa vijana.
Katika taarifa ilioambatana na siku ya wapendanao ya
Valentine-siku ambayo maafisa wa Thai utoa onyo kuhusu mapenzi ya ujana, wizara
ya afya ya uma ilionya kuwa magonjwa ya zinaa miongoni mwa wavulana wa miaka 10
hadi19 yameongezeka mara tano zaidi katika kipindi cha miaka 10 iliopita.
''Ni kwa sababu ni asilimia 43 ya vijana ndio wanaotumia
mipira ya kondomu na kwamba huchagua mipira ambayo ni mikubwa ikilinganishwa na
vipimo vyao huku wakiogopa kwamba watafanyiwa masikhara kwa kuwa wadogo''.
Wizara hiyo imeongezea kwamba inapanga kutumia dola millioni
1.4 mwaka huu ili kugawanya zaidi ya mipira millioni 43 kwa watu wote katika
ufalme huo.
Vijana katika ufalme huo hufunzwa kutofanya ngono badala
kuambiwa watumie kinga wakati wanapotekeleza tendo hilo.
No comments:
Post a Comment