Kombe la Mataifa ya Afrika
waziri wa michezo nchini Egypt Khaled Abdel-Aziz
amethibitisha kuwa nchi yake imetupilia mbali jitihada zake za kuwa mwenyeji wa
michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2017.
Anasema,tumeamua kujiondoa kwenye maombi hayo na tutawaunga
mkono Algeria.
Nchi za Gabon na Ghana ziliomba zabuni hiyo ,nalo
shirikisho
la soka barani Africa litatoa jina la mwenyeji wa michuano hiyo mnamo tarehe 8
ya mwezi April.
Libya nayo ilikuwa na tamanio la kuwa mwenyeji wa fainali za
michuano hiyo lakini ilijiondoa kutokana na hali ya kisiasa inayoendelea nchini
humo.
Waziri Abdel-Aziz hakufunguka zaidi kueleza sababu za ziada
za kujiondoa lakini imeshikilia msimamo huo baada ya mjumbe wa kamati ya
utendaji ya FIFA ,Hany Abu Rida kusema kwamba haina maana yoyote kwa nchi mbili
za kiarabu kushindania zabunia hiyo.
Anasema Egypt haitaweza kushindana na Algeria lakini tuna
hakikisha kutoa usaidizi makini kadiri tuwezavyo anahakikisha Abu Rida katika
maelezo yake.
Kujiondoa huko kunakuja baada ya vifo vya mashabiki 22 mnamo
tarehe 8 February wakati polisi na washabiki walipovaana kabla ya mchezo baina
ya timu ya Zamalek ya Cairo na ENPPI.
Kufuatia tukio hilo shughuli zote za soka za ndani
zimesimamishwa mpaka hapo itakapotangazwa tena lakini waziri mkuu wa Misri
Ibrahim Mahlab anaamini kuwa ligi ya nchi hiyo haitaishia kufutwa ingawa kwa
sasa tunaangalia zaidi suala la usalama michezoni na kupisha hali mbaya ya hewa
iliyotokea michezoni.
Waziri huyo ametoa ahadi ya kujadili suala hilo wiki ijayo
na kutilia mkazo vipaumbele vya mazungumzo hayo kuwa ni kuweka mambo katika
mizania na hasa ligi kurejeshwa tena na suala la usalama wa wanamichezo.
Na kama Ligi itaendelea basi washabiki hawatahitajika
uwanjani Mahlab ameelezea msimamo wa nchi yake.
Tukio hilo la hivi karibuni lililotokea katika mzunguuko wa
kwanza wa ligi nchini humo,ambalo linakuja na amri ya kutoruhusu mashabiki
uwanjani ili kunusuru usalama mchezoni,ikumbukwe kwamba tangu February mwaka
2012 mashabiki walipigwa marufuku kushuhudia mechi zikipigwa uwanjani kutokana
na washabiki takribani sabini na wawili wa Al Ahly walipovaana na mashabiki wa
timu ya Al Masry katika uwanja wa Port Said na kusababisha maafa hayo.
No comments:
Post a Comment