Pages

Wednesday, February 18, 2015

Moto wateketeza msitu wa hifadhi ya taifa Jozani kisiwani Zanzibar.


Hekta zipatazo 17 ziliziomo ndani ya hifadhi ya taifa ya msitu wa Jozani kisiwani Zanzibar zimeteketea kwa moto ambao unasadikiwa umetokana na wavunaji haramu wa asali.

Moto huo umeweza kudhibitiwa  na vikosi vya ulinzi na uokozi na wafanyakazi wa wizara yakilimo kwa kushirikaina na wananchi  kutokana na magari ya zimamoto kushindwa kufika ndani zaidi ya msitu ambapo hekta hizo 17 zimeathirika kati ya heta 5000 zilizopo katika msitu huo wa Jozani ambao pia ni maarufu kwa watalii.




Kutoakna na moto huo makamu wa pili wa rais balozi Seif Ali Iddi alifika katika msitu huo nakujionea athari za moto huo wenye hadhi kubwa kwa Zanzibar kutokana na mazingira ya miti yake na wanyama adimu duniani ambapo akizungumza na watendaji wa wizara balozi Seif mbali ya kuwapongeza wananchi na askari kwa kudhibiti moto huo amesema ikohaja ya hatua zamaksudi kuchukuliwa dhidi ya wavunaji hao haramu ambao wamekuwa kero karibu misitu hata kiswani Pemba.


Mapema katibu mkuu wizara ya kilimo Afan Othman katibu alisema unyevunyevu uliopo kwenye eneo hilo nao umechangia kuepusha athari zaidi za kuenea kwa moto huo kwa kutoathiri miti mikubwa na msitu huo pia nitegemezi kubwa kwa wakulima wa mpunga, naye mkuu wa kikosi cha zimamoto na uokozi wa mkoa wa kusini Unguja SSF Shaban Ramadahn Ali amesema bado kikosi kina uhaba mkubwa wa vifaa vya kisasa na magari yenye uwezo wakukabiliana na maafa yaaina hiyo


Hifadhi ya taifa ya msitu wa Jozani imekuwa maarufu kimataifa kutokana na maumbile yake ya kuwa na viumbe mchanganyiko wakiwemo wanyama adimu kama Kima Punju, Paa nunga, Nguruwe, Vipepeo na aina mchanganyiko ya ndege na miti mbalimbali.

No comments:

Post a Comment