Mlipuko
Jeshi la Marekani linasema kuwa mtaalamu mmoja wa silaha za
kemilkali aliyekuwa akifanya kazi na kundi la Islamic State ameuawa kwenye
mashambulizi ya muungano nchini Iraq.
Marekani inasema kuwa kifo cha mwanamume huyo kwa jina Abu
Malik kitavuruga uwezo wa kundi hilo
wa kuunda na kutumia silaha za kemikali.
Abu Malik anaripotiwa kufanya kazi kama mtaalamu wa silaha
za kemikali kwa rais wa zamani wa Iraq Sadam Hussein kabla ya uvamizi
ulioongozwa na Marekani mwaka 2003.
Kundi la Islamic State hudhibiti maeneo makubwa nchini Syria
ambapo serikali imekuwa ikiharibu silaha za kemikali.
No comments:
Post a Comment