Wabunge wa bunge la Uingereza wameunga mkono sheria
inayoruhusu uzaaji wa wa watoto wenye vinasaba, DNA kutoka kwa wanawake wawili
na mwaume mmoja, katika tukio la kihistoria.
Uingereza kwa sasa itakuwa nchi ya kwanza kuweka sheria
zinazoruhusu watoto wenye vinasaba vya watu watatu tofauti.
Katika kura iliyopigwa katika bunge la Commons, wabunge 382
waliunga mkono muswada huo wa sheria na wabunge 128 walipinga mbinu inayozuia
magonjwa ya kijenetiki kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Wakati wa mjadala huo, mawaziri wamesema mbinu hii ni
"mwanga kwa safari ndefu ya giza" kwa familia kupata watoto.
Upigaji kura zaidi unahitajika katika baraza la bunge la
juu, maarufu kama House of Lords. Iwapo kila
kitu kitakwenda sawa, basi mtoto
wa kwanza wa teknolojia hii atazaliwa mwaka ujao.
Watetezi wa mpango huu wanasema uungwaji mkono wa sheria hii
"ni habari njema kwa maendeleo ya tiba" lakini wakosoaji wanasema
wataendelea kupinga mpango huu ambao una mashaka mengi kuhusu maadili na
usalama katika uzazi huu.
Makisio yanasema watoto 150 wanaopatikana kutokana na
vinasaba vya watu watatu watazaliwa kila mwaka.
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron anasema:
"Hatuzungumzii Mungu hapa, tunahakikika kuwa wazazi wawili ambao wanataka
mtoto mwenye afya wanaweza kumpata."
Mpango huu ambao umebuniwa Newcastle, utasaidia wanawake
kama Sharon Bernardi, kutoka Sunderland, ambaye alipoteza watoto wote saba kutokana
na ugonjwa wa mitochondrial.
No comments:
Post a Comment