Mamlaka nchini Saudi Arabia kwa mara nyengine tena
imeahirisha adhabu nyengine ya viboko dhidi ya mwanablogu Raif Badawi.
Hakuna sababu iliotolewa,lakini awamu mbili za kutoa adhabu
kama hiyo hapo awali ziliahirishwa kutokana na sababu za kiafya.
Bwana Badawi amepewa hukumu ya viboko 1000 pamoja na
kuhudumia kifungo cha miaka 10 jela kwa kutusi Uislamu.
Raif Badawi na familia yake
Mwanaharakati wa Saudia ambaye pia ni wakili Suad
al
Shammary ambaye alifanya kazi na bwana Badawi katika blogi yake ameachiliwa
huru.
Alizuiliwa kwa miezi mitatu bila kufunguliwa mashtaka kuhusu
matamshi aliotoa katika mtandao wa Twitter ambayo wapinzani wake walisema
yanapinga Uislamu.
No comments:
Post a Comment