Mwanafunzi mmoja wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Idara ya sheria mwaka wa pili, Mathias Thimoth ametiwa mbaroni kwa tuhuma za wizi wa kompyuta mpakato ya mwanafunzi mwenzake.
Habari zaidi zinasema kwamba wanafunzi wengi chuoni hapo walikuwa wakiibiwa kompyuta, hivyo wakaweka mtego ndipo mwananfunzi huyo alipodakwa redi hendedi na mali hiyo.
Hata hivyo, mara baada ya kukamatwa mwanafunzi huyo aliruka kimanga akidai kuwa yeye hahusiki na wizi wa kifaa hicho na akadai kwamba amebambikiziwa.

No comments:
Post a Comment